BASI LAUA WATU 11 LIKITOKA KIGOMA KWENDA KAHAMA...RAIS MAGUFULI ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI

Watu 11 wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa kutokana na ajali ya gari aina ya hiece kugongana na malori matatu katika kijiji cha Mubigera kata ya Nyantakara wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera wakati wakisafiri kutoka wilaya ya Kibondo kuelekea Kahama mkoani Shinyanga.



Mganga mkuu wa hospitali teule ya Biharamulo Dr. Grasmus Sebuyoya amethibitisha kupokea miili ya watu hao wakiwa maiti na majeruhi sita na kwamba kati ya majeruhi hao wawili hali zao ni mbaya na waliofariki wa jinsia ya kiume ni saba na jinsia ya kike ni watatu

Dr. Sebuyoya amewataja waliojeruhiwa kuwa ni Juma Samo (25) Joseph Otieno (30), Oscar Leonard Sebastian (27), Baseke Mashinga Nyabashiki (31), Mahalulo Charles (25) na majeruhi wa sita hajafahamika kwa kuwa hajajitambua na kwamba maiti waliofia eneo la tukio ni Tisa na wawili wamefariki baada ya kufikishwa hospitalini hapo.

Awali Mwenyekiti wa kijiji cha Mubigera,Mapunda Kayuki amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya Saa 11 jioni ambapo hiece ilitaka kukwepana na roli kwenye barabara ya Biharamulo kwenda Kahama kwenye kijiji hicho na kugongana ambapo dereva wa Hiece na tingo wake ni miongoni mwa waliofariki.


Bw Kayuki amesema hiece hiyo yenye  namba za usajili T.542 DKE ilikuwa ikitokea kibondo kwenda kahama ambapo maroli yaliyohusika kwenye ajali hiyo ni T.860CGS, T.103 DUJ na T.147 DUJ magari  yako chini ya usalama wa jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi.


Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera Agustino Olomi amesema hajakamilisha taarifa kamili ya tukio hilo ikiwa ni pamoja na kutambua majina ya waliopoteza maisha mpaka ajiridhishe na taarifa,  zitatolewa kwa umma bila kutia mashaka ili ndugu wa marehemu waweze kujua na kufuatilia kwa uhakika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527