BAADA YA BIASHARA YA KARANGA,DIAMOND KUFUNGUA RADIO NA TV MWEZI UJAO



Kampuni ya Wasafi Classic (WCB), inayomilikiwa na msanii maarufu wa muziki wa Bongofleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ wanatarajia kufungua televisheni na redio Februari mwaka huu.
Haya yamebainika ikiwa ni saa chache tangu Diamond na viongozi wa kampuni hiyo watupie jumba la kifahari  ambalo linaelezwa  litakuwa ndiyo ndiyo makao makuu ya WCB ambapo mbali ya kuwa na studio za kurekodia muziki pia litakuwa na Redio na TV.
Mwananchi ilimtafuta mmoja wa mameneja wa Diamond, Said Fela  kuweza kujua hasa ni lini TV na redio hizo zitaanza kufanya kazi alisema itaanza rasmi Februari mwaka huu.
Katika mahojiano hayo, Fela amesema hatua waliofikia ni katika harakati za kampuni hiyo kuendelea kujitanua na kutoa fursa kwa vijana wengi zaidi.
Fela amesema pamoja na kwamba wao ni watu wanaojishughulisha na kazi za burudani, lakini TV yao na redio zitakuwa zinarusha vipindi vya aina zote vikiwemo vya kuelimisha na habari kama vilivyo vituo vingine.
“Kwetu sisi hii tunaona ni hatua nzuri kwa kuwa tunajua tukifungua vituo hivi ndivyo kadri tunavyozidi kuzalisha ajira na tumeamua kutumia wataalam ambao walikuwa kwenye fani hiyo ikiwemo wazee waliostaafu katika Shirika la Utangazaji(TBC) enzi hizo TVT kwa ajili ya kutuongoza kwa kuwa sisi wenyewe hatuwezi,”amesema Fela.
Hata hivyo, alipoulizwa kama wamejenga wenyewe mjengo huo au Fela amesema wamekodisha kama walivyokuwa wamekodisha ile ya Sinza huku sababu za kuhama akieleza ni kutokana na kuongeza huduma na pia sehemu waliyokuwepo kulikuwa na taabu ya maegesho ya magari na kujaa maji hasa mvua zinaponyesha.
Mjengo huo wa wasafi wa ghorofa moja ambao upo maeneo ya Mbezi umeonekana kuwa gumzo leo Alhamisi katika mitandao ya kijamii na watu wengi wamempongeza Diomond na uongozi wake kwa hatua aliofikia.
Mbali na redio, tayari Diamond ameshajiingiza katika biashara nyingine ikiwemo ya manukato yanayoitwa 'Chibu', na 'Diamond karanga' 
 Na Nasra Abdallah, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527