SASA BUNGE KUMNG'OA MUGABE....KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NAYE KURINDIMA

Rais Mugabe anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa umma na chama chake cha Zanu-PF

Chama cha rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kinatarajiwa kuanza mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa na imani nae.

Afisa wa Zanu-PF amesema kuwa hoja ya kumnyang'anya urais itawasilishwa bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumg'oa madarakani unaweza kuchukua siku mbili tu.

Mashtaka yaliyomo kwenye hoja hiyo ni pamoja na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 "kumpa madaraka makubwa ya kikatiba mkewe Grace, na kushindwa kuheshimu katiba''.

Viongozi wa kijeshi , ambao wiki iliyopita waliingilia kati kuchukua mamlaka ya nchi walisema atakutana na makamu wake wa rais wa zamani aliyeuhamishoni karibuni.

Jeshi limesema kuwa lina mpango na Mugabe kuhusu hali ya baadae.

Jumapili , licha ya shinikizo kubwa Bwana Mugabe aliwashangaza wengi kwa kukataa kujiuzulu, na badala yake katika hotuma yake kupitia televisheni alisema kuwa ataongoza mkutano mkuu wa chama Zanu-PF.
Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527