KAULI YA MAMA KANUMBA BAADA YA LULU KUHUKUMIWA JELA MIAKA MIWILI

Mama wa Muigizaji Marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa amefunguka na kusema kwamba leo atakwenda makaburi ya Kinondoni alipozikwa mwanaye ili kwenda kumzika upya.



Mama Kanumba ametoa kauli hiyo muda mfupi baada ya Mahakama Kuu kumhukumu kifungo cha miaka miwili Muigizaji Elizabeth Michael ambaye alikuwa mtuhumiwa katika kesi ya mauaji bila kukusudia yaliyopelekea kifo cha muigizaji huyo.


“Namshukuru Mwenyenzi Mungu, naishukuru Mahakama imetenda haki, naishukuru Serikali yangu awamu ya tano“

“Kalale salama mwanangu Steven Kanumba na nikitoka hapa nakwenda makaburini naamini nakwenda kumzika akapumzike kwa amani” Mama Kanumba


Kwa upande wa Wakili wa Muigizaji Lulu Peter Kibatala ameweka wazi kwamba watakata rufaa kufuatia hukumu ya Mahakama iliyotolewa leo kwa mteja wake.


Muigizaji Lulu leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua muigizaji mwenzake ambaye pia alikuwa mpenzi wake Steven Kanumba usiku wa Aprili 7 2012.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527