DED BARIADI AMVUA MADARAKA MKUU WA SHULE KWA KUFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI WAKE



Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Abdalah Malela amemvua madaraka Mwalimu Mkuu Masunga Ng’waya wa Shule ya Msingi Mwashagata, iliyopo kijiji hicho kata ya Ihusi kwa kosa la ukosefu wa maadili.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, mkurugenzi huyo alisema tukio hilo lilitokea hivi karibuni la baada ya mwalimu mmoja wa shule yake kumrubuni mwanafunzi wake kwa kufanya mapenzi naye tena kwenye nyumba yake, kitendo ambacho ni cha kukosa maadili.

“Imebainika hili ni tukio la nne kwa mwalimu huyo kutuhumiwa kufanya mapenzi na wanafunzi tofauti tofauti lakini amekuwa hachukuliwi hatua, lakini mimi kwa mujibu wa sheria nimemvua madaraka mwalimu mkuu huyo ili awe mwalimu wa kawaida, sababu amekosa maadili ya kuendelea kushika wadhifa huo,” alisema mkurugenzi huyo.

Aidha, alisema kesi hiyo tayari imefikishwa polisi na wakati wowote mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani. Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Festo Kiswaga alisikitishwa na kitendo hicho na kumtaka mkurugenzi wa halmashauri hiyo kumchukulia hatua na kuwashauri wazazi wamuache mwanafunzi huyo aendelee na masomo yasije yakampita huku hatua za kisheria kwa mtuhumiwa zikiendelea.

Mlezi wa mwanafunzi huyo, alisema mwanawe alisimama masomo kwa muda wa wiki mbili kutokana na tukio hilo.

 Mwalimu Ng’waya alipozungumza na mwandishi wa habari kwa njia ya simu alikiri kuvuliwa madaraka na kueleza amekuwa mwalimu wa kawaida huku akiendelea kufundisha katika shule hiyo.
Chanzo-Habarileo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527