TACOSODE WATOA DIRA YA KUTATUA CHANGAMOTO ZA SEKTA YA AFYA


Mkurugenzi wa Miradi wa Tacosode, Theofrida Kapinga akizungumza jambo wakati wa semina iliyofanyika katika ukumbi wa Valentine mkoani Iringa
Afisa mchechemzi wa mradi Abrahm Kimuli akiendelea kutoa elimu kwa wanasemina walikuwa wamehudhuria katika ukumbi wa valentine 
Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye mijadala ya sekta ya afya na jinsi gani wanaweza kutatua changamoto zinazoweza kuikoa sekta ya afya hapa nchini -Picha na Fredy Mgunda,Iringa.

***
BARAZA la Vyama vya hiari na Maendeleo ya Jamii (TACOSODE) limesema wananchi wamekuwa na uelewa kuhamasisha bajeti kuwa na kipaumbele kwa changamoto zinazowakabili.


Hayo ameyasema Mkurugenzi wa Miradi wa TACOSODE, Theofrida Kapinga wakati akizungumza semina ya kujadilia
jinsi gani ya kutatua changamoto zinazoikumba sekta ya afya iliyofanyika katika ukumbi wa Valentine Manispaa ya Iringa.


“Zamani wananchi hata viongozi wa sekta ya afya walikuwa wagumu kuelezea changamoto zinazowakabili
lakini saizi wananchi na viongozi wamekuwa na elimu ya kutosha juu ya kueleza changamoto zilizopo katika sekta hiyo ndio maana vitu vingi vinaibuka muda huu”,
alisema Kapinga.


Kapinga alisema licha ya serikali kufanya juhudi kutatua changamoto ili kuto huduma ya afya bora lakini
bado sekta hiyo inaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo zinakwamisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi.

“Ukiangalia tafiti nyingi zinaonyesha kuwa serikali imekuwa ikishindwa kuongeza bajeti ya sekta ya afya ili kufikia asilimia 15 ya bajeti yote ya serikali kwa kuzingatia azimio la Abuja”,alisema Kapinga.

Aidha Kapinga alisema moja ya changamoto kubwa ni uhaba wa kupatikana kwa dawa muhimu,vitendanish na
vifaa tiba kulinganisha na utafiti wa mwaka 2012 ulifanywa na taasisi ya afya ya Ifakara na kugundua kuwa asilimia 41 ya dawa muhimu zinahitajika kwa kiasi
kikubwa.


Kwa upande wake afisa mchechemzi wa mradi Abrahm Kimuli aliwataka watumishi wa sekta ya afya kuzibaini changamoto zinazowakabili na kuzitafutia ufumbuzi kushirikiana na serikali panoja na sekta binafsi.

“Unajua kweli kuna changamoto
nyingi ambazo zinawakabili hivyo ni lazima muwe wabunifu kuzitafutia ufumbuzi lakini kwenye hizi sekta binafsi kuwa wasomi wengi ambao wanaweza kutoa ushauri
mzuri wa kutatua changamoto zilizopo” alisema Kimuli 

Kimuli alisema wananchi wamekuwa na uelewa wa maswala ya afya kutokana na elimu waliopata katika mradi
wa uhamasishaji wananchi kushiriki katika masuala ya afya katika kuangalia vipaumbele vya bajeti uliokuwa ukitekelezwa katika Mikoa ya Iringa pamoja na
Dodoma.


Alisema kuwa wananchi mradi huo katika utekezwaji wake katika Halmashauri ya Iringa pamoja na Kongwa mkoani
Dodoma wananchi wamekuwa na mwamko katika masuala ya afya ushiriki kwa kuchangia katika huduma za afya.

Kimuli alisema mradi huo wa miaka minne umekuwa na matokeo katika wilaya ambazo umetekelezwa kwa
wananchi kuwa na mwamko katika masuala ya huduma za afya kwa kuchangia hata nguvu zao pale panapobidi.

Aidha amesema mradi huo ukiisha wanaweza kufanya katika sekta zingine ili kuwa maendeleo ya katika masuala mbalimbali kutatuliwa.

Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Iringa Abel Mgimwa alisema kuwa serikali ya awamu ya tano imejipanga kuahakikisha changamoto zinatatuliwa kimkakati kulinga na bajeti wanayokuwa wameipanga.


“Ukiangalia bajeti ya mwaka wa fedha mwaka huu imepanda hivyo ni dalili njema za kuanza kutatua changamoto ambazo zimekuwa zikidumu kwa miaka mingi na kuwaomba wananchi na viongozi kuwa na subira katika kipindi hiki cha utatuzi wa changamoto hizo”, alisema Mgimwa.

Mgimwa aliwapongeza TACOSODE
kwa mchango wao katika sekta ya afya ambayo imekuwa na changamoto nyingi hivyo sio rahisi kwa serikali kutatua kwa haraka hivyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527