
Mbunge
wa Arusha Mjini, Godbless Lema amesema kuwa baraza jipya la mawaziri
lililotangazwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John
Magufuli halina jipya kwani sura zilizobaki ni zile zile.
Ameyasema
kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa Twitter, ambapo amesema kuwa
ameona mabadiliko ya baraza la Rais Magufuli lakini bado fikra ni zile
zile na watu ni wale wale na kudai katiba mpya ndio suluhisho la vyote.
“Nimeona
Mabadiliko ya baraza la JPM. Watu ni wale wale, fikra zile zile. Katiba
Mpya yenye fikra mpya ndio tumaini kwa mabadiliko sahihi ya nchi na
watanzania kwa ujumla,”ameandika Lema
Social Plugin