SPIKA WA BUNGE AAGIZA ZITTO KABWE NA SAED KUBENEA WAFIKISHWE MBELE YA KAMATI SAKATA LA RISASI ZA TUNDU LISSU

Spika wa Bunge, Job Ndugai amemuagiza kutafutwa kwa namna yoyote Mbunge wa Ubungo(Chadema), Saed Kubenea apelekwe kesho kwenye Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama ili ahojiwe kuhusu kauli aliyoitoa ya kumtuhumu Spika kuwa amedanganya idadi ya risasi alizopigwa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.


Pia Spika Ndugai ameagiza Kubenea na Mbunge wa Kigoma Mjini(ACT Wazalendo), Zitto Kabwe kupelekwa katika Kamati ya Bunge ya Maadili na Madaraka kwa tuhuma mbili tofauti 


Zitto anatuhumiwa kutamka kuwa Bunge limewekwa mfukoni na muhimili fulani, wakati Kubenea ni kwa kumtuhumu Spika kusema uongo wa idadi ya risasi alizopigwa Lissu.


Spika Ndugai ametoa maagizo hayo bungeni mjini Dodoma leo Jumanne.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527