POLISI: BETRI ZA SOLA NDIYO CHANZO CHA MOTO KUUNGUZA NYUMBA YA ZITTO KABWE

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui amesema kuongezeka joto katika betri za sola ndio chanzo cha moto uliounguza Nyumba ya Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe juzi jioni.


Nyumba hiyo ipo mtaa wa Kibingo, mji mdogo wa Mwandiga katika wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma.


Amesema joto hilo limesababisha mlipuko wa moto kwenye betri za sola na hivyo nyumba kushika moto na kuteketea yote.


Polisi wanamshikilia mlinzi wa nyumba hiyo, Norbert Joseph kwa mahojiano zaidi ili kubaini kama kuna uzembe wowote uliofanywa na kusababisha moto kuwaka.


Msaidizi wa Zitto anayeifahamika kwa jina la Nyembo Mustafa ametaja thamani ya hasara iliyosababishwa na moto huo kwamba ni Sh 45 milioni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527