Makubwa Haya: AMUUA MWENZAKE WAKIBISHANA KUHUSU MAKALIO MAKUBWA YA MWANAMKE


NB-Siyo mwanamke aliyesababisha kifo

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaizidizi Jonathan Shanna Warioba, ametoa onyo kali kwa wananchi wenye tabia za udhalilishaji kwa wanawake kuacha tabia hiyo mara moja huku akisema kwamba udhalilishaji umesababisha kifo.



Kamanda Shanna amelazimika kusema hayo hayo wakati akitolea ufafanuzi juu ya tukio la mauaji ya mkazi wa Kijiji cha Vilabwa Wilaya ya Kisarawe Imma Habibu ( 26).


Kwa mujibu wa Shanna Marehemu aliuawa juzi majira ya saa mbili asubuhi wakati walipokuwa kijiweni na wenzake baada ya kutokea ugomvi kati yake na Ramadhani Habibu (23) ambaye ni ndugu yake, baada ya mwanamke mmoja ambaye anadaiwa kuwa na maumbile makubwa (makalio) kupita, mbele yao.


Alisema baada ya mwanamke huyo kupita mbele yao walianza mabishano ambapo marehemu alisema mwanamke huyo ana makalio makubwa na Ramadhani alisema ni makalio ya kawaida sio makubwa.


Kamanda Shanna alieleza kuwa baada ya mabishano hayo ndipo ulipozuka ugomvi hadi kufikia hatua ya Ramadhani kumuua kaka yake kwa kumchoma kisu kifuani upande wa kuliana na alifariki dunia akiwa njiani anapelekwa hosptali ya kisarawe.


Alisema jeshi la polisi linamshikilia mtuhumiwa kwa kufanya mauaji hayo na kuwa atafikishwa mahakamani mara moja na kuwa amekubali kuwa amefanya mauaji hayo.


Kufuatia,tukio hilo kamanda Shanna aliendelea kutoa onyo kwa wananchi na vijana wanaoshinda vijiweni kuacha tabia ya udhalilishaji hasa kwa wanawake na kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria na kuwa kama kuna mtu aliyefanyiwa vitendo vya namna hiyo atoe taarifa polisi na atafikishwa mahakamani.


"Wito kwa wale wanaokiuka haki za binadamu kwa kumdhalilisha mtu waache mara moja, mfano kisheria hata kumkonyeza mtu ni kosa la jinai hivyo unapaswa kufika polisi, na tutamfuatilia kisha kumpeleka mahakamani" Kamanda Shana amefafanua


Pia kamanda Shanna ametoa rai kwa wanawake kuvaa nguo zinazositiri maungo yao ili kuepusha vishawishi na matamanio kwa wanaume

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments