POLISI WAUA JAMBAZI ALIYEVAMIA BENKI KWA KUTOBOA UKUTA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Tarime Rorya lililazimika kutumia risasi za moto kumdhibiti mtu mmoja ambaye alivamia Bank ya NBC usiku akidaiwa kuingia baada ya kutoboa ukuta.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime Rorya Henry Mwaibambe amesema Jeshi hilo linaendelea kufanya uchunguzi kuhusu mtu huyo ambaye hakufahamika jina wala umri ambaye alivamia Bank hiyo mara mbili.

”Jeshi la Polisi linaendelea kufanya uchunguzi wa tukio la ajabu kidogo. Tarehe 19, Saa Sita na dakika Nne usiku, mtu mmoja ambaye hakufahamika jina lake wala umri amefariki dunia baada ya kujeruhiwa kwa risasi na askari Polisi waliokuwa kwenye lindo la Bank ya NBC.” – Kamanda Mwaibambe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527