HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO KWA AWAMU YA PILI MWAKA 2017




TAARIFA KWA UMMA
Ofis ya-TAMISMI inapenda kuwajulisha wananchi juu ya orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa awamu ya pili kwa mwaka 2017. Wanafunzi hawa wataanza muhula wa kwanza na masomo tarehe 24 Agosti,2017, na hakutakuwa na mabadiliko yeyote ya shule. Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangiwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti hadi tarehe 08 Septemba 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kuripoti ,atakuwa amepoteza nafasi.


Mwanafunzi mara uonapo jina lako kwenye tovuti ya ofisi ya Rais TAMISEMI kwamba umechaguliwa kujiunga na kidato cha tano inabidi kudowlod fomu ya kujiunga na shule husika kwenye mtandao..


Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya ufundi awamu ya pili mwaka 2017 pamoja na fomu za kujiunga na shule (joining instructions) inapatikana kwenye tovuti ya Ofisi Ya Rais TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz


Imetolewa na,
Katibu Mkuu
Ofisi Ya Rais-TAMISEMI
23 Agosti 2017


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527