WAZIRI MWAKYEMBE AWASHUKURU WATANZANIA KWA USHIRIKIANO WALIOMPA MSIBA WA MKE WAKE

Leo Jumatano ya July 26 ikiwa ni siku 11 zimepita tangu utokee msiba wa mke wa waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo Dr Harrison Mwakyembe, leo ameongea na vyombo vya habari nyumbani kwake Kunduchi Dar es Salaam.


Mwakyembe amewashukuru Watanzania kwa ushirikiano mkubwa waliompa katika kuombeleza kifo cha mkewe Linah Mwakyembe kilichotokea usiku wa Julai 15 mwaka huu kwenye Hospitali ya Aga Khan.


Dk Mwakyembe pia amemshukuru Rais John Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa mchango mkubwa walioutoa katika kumuuguza mkewe.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527