RAIS WA TFF JAMAL MALINZI NA WENZAKE WARUDISHWA RUMANDE TENA HADI JULAI 31


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa wamerudishwa rumande kwa mara nyingine kutokana na upelelezi wa kesi yao kutokamilika hivyo wamerudishwa tena Mahakamani Julai 31 mwaka huu shtaka lao litakaposomwa tena.


Uamuzi huo umetolewa katika Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es Salaam, ambapo ndipo mashtaka hayo yalifunguliwa mara ya kwanza na kuendelea mpaka sasa.


Malinzi na Mwesigwa walishikwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mnamo Juni 27 kwa kutuhumiwa na matumizi mabaya ya madaraka waliyokuwa nayo katika uongozi wao na kupandishwa mahakamani kwa mara ya kwanza mnamo Juni 29 na kusomewa mashtaka 28 yakiwemo kughushi na kutakatisha fedha kupitia akaunti ya TFF.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527