AMUUA MKE WAKE KWA KUMCHOMA KISU KIFUANI



POLISI mkoani Morogoro inawashikilia watu tisa kwa tuhuma tofauti akiwemo mkazi wa Kijiji cha Chingholwe, Kata ta Chanjale wilayani Gairo, Bahati Malima kwa kumuua mkewe Janet Sajilo (35) kwa kuchoma na kitu chenye ncha kali sehemu ya kifuani na kufariki dunia papo hapo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Ulrich Matei alisema jana kuwa mauaji hayo yalifanyika juzi saa sita eneo la Kijiji cha Chingholwe, Kata ya Chanjale, Tarafa ya Nongwe. Kamanda Matei alisema chanzo cha tukio hilo ilidaiwa ni wivu wa mapenzi.

Alisema baada ya mtuhumiwa kumchoma mkewe na kitu chenye ncha kali kifuani, alifariki dunia papo hapo baada ya kuvuja damu nyingi. 

Hata hivyo, alisema chanzo halisi kilichosababisha mume huyo kuchukua uamuzi wa kumchoma mkewe na kitu chenye ncha kali kifuani, hakijafahamika na uchunguzi zaidi unaendelea na hatua za kumfikisha mtuhumiwa mahakamani zitafuatwa.

Aidha, Haji Athuman (28) ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Makambako, Mkoa wa Njombe anashikiliwa na Polisi akiwa na simu aina mbalimbali zipatazo 748. Simu hizo ni Tecno, Itel na Ditel pamoja na betri za simu 650 na chaja za simu 830.

IMEANDIKWA NA JOHN NDITI - HABARILEO MOROGORO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527