MFAHAMU MTANZANIA ANDREW CHENGE AMBAYE ANAHUSISHWA KWENYE KASHFA NYINGI ZA KIFISADI TANZANIA


Andrew Change alizaliwa Tanganyika Tarehe/Mwezi/Mwaka 24/12/1947 . Kwa sasa ana miaka 69. Andrew Chenge ni Mbunge wa Bariadi taangu 2005.

KAZI NA TEUZI MBALIMBALI​
2005-Sasa -mbunge Bariadi magharibi na Mwenyekiti wa Bunge

2006-2008 Aliteuliwa kuwa waziri wa Miundombinu alijiuzulu mwaka 2008 kwa kashifa ya kumiliki account Nje ya Nchi iliyokua na Kiasi cha $1,000,000 ambazo ni sawa na sh. 1billion kwa kwa wakati huo ambazo zilihusiana na kashifa ya Rada. Baadaye TAKUKURU wakachunguza na Kuja na jibu kuwa Chenge hausiki.

January 6,2006-October 2006 
Aliteuliwa kuwa waziri wa Ushirikiano wa Africa Mashariki

2005 alichaguliwa na Wananchi wa Bariadi kuwa Mbunge

1993-1995 Rais Ali Hasan mwinyi alimteua kua mwanasheria mkuu wa serikali Alichaguliwa kuwa mwanasheria mkuu wa serikali (AG)

1995-2005 Rais Benjamin Mkapa alimteua Andrew Chenge kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali wadhifa aliodumu nao kwa miaka mingine 10.

2009- Chenge akiendesha gari Jijini Dar es Salaam alimgonga mkazi wa Dar es Salaam na Kumsababishia Kifo ambapo alipigwa fine ya Sh. 700,000/= kama adhabu.

Mwaka 2015 Wananchi wa Bariadi walimchagua tena Chenge.


ELIMU YAKE:

LLB (UDSM)
LLM (Harvard)​

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments