WAANDAAJI WA SHINDANO LA MISS TANZANIA KUBURUZWA MAHAKAMANI


Kurugenzi ya Sheria ya Mtandao wa Wanafunzi Tanzania TSNP imekusudia kuwasilisha kwa kampuni inayoandaa MISS TZ notisi ya madai na kusudio la kuwafikisha Mahakamani kama watashindwa kuwalipa washindi wa MISS TZ 2016.

Hatua hiyo inakuja baada ya Kurugenzi hiyo kupokea malalamiko kutoka kwa mamiss walioshiriki Miss Tanzania 2016 na kushinda nafasi za 2, 3 na 4 kutolipwa fedha zao walizoahidiwa na waandaaji wa mashindano hayo Lino International Agency Ltd.

TSNP imewataja washindi hao kuwa ni Mary Peter Clavery (Miss TZ 02), Grace Christopher Malikita (Miss TZ 03) na Anna Nitwa (Miss TZ 04) ambapo tayari mawakili wemepitia mikataba yao na kujiridhisha kuwa waandaaji wamekiuka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527