TAARIFA ZA ORODHA YA MAJINA YA ASKARI POLISI WANAODAIWA KUWA NA VYETI FEKI


Jeshi la Polisi nchini limekanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikiwahusisha askari wake kuwepo katika majina ya vyeti feki na kusema taarifa hizo ni za uongo na wala hazijatolewa na Jeshi hilo.


Hayo yamebainishwa na taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi, ACP Advera Bulimba na kusema wanaendelea kumtafuta mtu aliyesambaza taarifa hiyo kwa lengo la kupotosha umma ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yake na kuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia kama hiyo.


"Jeshi la Polisi nchini, linaujulisha umma kwamba, orodha ya majina ambayo yamekuwa yakisambazwa kwenye mitandao ya kijamii yakidai kuwa ni majina ya askari wa jeshi la polisi wenye vyeti feki ni ya uongo na wala taarifa hiyo haijatolewa na jeshi la polisi". Ilisema taarifa hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527