Picha: RAIS MAGUFULI AKABIDHI HATI KWA WAFANYAKAZI BORA ACACIA,WASHIRIKI MAANDAMANO MEI MOSI 2017



Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limewatunuku hati ya Mfanyakazi Bora wafanyakazi watatu kutoka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu na Buzwagi inayomilikiwa na Kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia.

Waliotunukiwa hati ya mfanyakazi bora 2017 na zawadi ya shilingi milioni 1.5 kila mmoja ni Elisante Okuli Mungure kutoka mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu,Masule Sangalali na Shaban Nassoro Katala kutoka mgodi wa Buzwagi. 

Wafanyakazi hao wamekabidhiwa hati hizo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Siku ya Wafanyakazi Duniani ‘Mei Mosi 2017’ambayo kitaifa imefanyika katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika mjini Moshi mkoani Shinyanga. 

Bwana Elisante Okuli Mungure anafanya kazi Huduma za kitaalamu kwenye uchimbaji wa madini (Technical Service) katika mgodi wa Bulyanhulu na Masule Sangalali ni Fundi mitambo katika mgodi wa Buzwagi wakati Shaban Nassoro Katala anafanya kazi ya uchimbaji katika mgodi wa Buzwagi. 

Wafanyakazi hao wametunukiwa hati ya mfanyakazi bora na TUCTA kwa ajili ya kazi bora,utii na kufuata maongozi sahihi katika kutimiza wajibu wa ujenzi wa taifa la Tanzania mwaka 2017. 

Wafanyakazi wa Acacia wameshiriki siku ya wafanyakazi duniani ‘Mei Mosi 2017’ kwa kufanya maonesho ya kazi wanazofanya mgodini lakini pia wameshiriki maandamano yaliyofanywa na wafanyakazi nchini mbele ya rais Magufuli. 

Nimekuwekea hapa chini picha za matukio yaliyojiri wakati wa siku ya wafanyakazi duniani leo Jumatatu Mei Mosi 2017.
Bwana Elisante Okuli Mungure kutoka mgodi wa Bulyanhulu akipokea hati ya Mfanyakazi bora mwaka 2017 katika viwanja vya ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa sherehe za Mei Mosi.
Baadhi ya wafanyakazi kutoka mgodi wa Bulyanhulu wakifurahia baada ya mfanyakazi mwenzao Elisante Okuli Mungure kutajwa kuwa ni Mfanyakazi Bora mwaka 2017 


Elisante Okuli Mungure akionesha hati aliyopewa
Elisante Okuli Mungure akiwa katika banda la mgodi wa Bulyanhulu
Kulia ni bwana Masule Sangalali ambaye ni fundi mitambo katika mgodi wa Buzwagi na Shaban Nassoro Katala anayefanya kazi ya uchimbaji katika mgodi wa Buzwagi wakionesha hati zao za Mfanyakazi Bora mwaka 2017
 Masule Sangalali na Shaban Nassoro Katala wakionesha hati zao za ushindi
Kushoto ni Elisante Okuli Mungure kutoka mgodi wa Bulyanhulu ,katikati ni Masule Sangalali na Shaban Nassoro Katala wakionesha hati zao za ushindi

Wafanyakazi wa kampuni ya Uchimbaji madini  ya Acacia inayomiliki migodi ya dhahabu ya Buzwagi,North Mara na Bulyanhulu wakiwa wamebeba bango wakati wa sherehe za Mei Mosi 2017 katika viwanja vya Ushirika Moshi mkoani KilimanjaroRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea maandamano ya wafanyakazi katika viwanja vya Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa sherehe za Mei Mosi mwaka 2017.

Wafanyakazi wa kampuni ya Uchimbaji madini  ya Acacia wakiandamana kwenye sherehe za Mei Mosi 2017
Bango likiwa na kauli mbiu ya Mei Mosi 2017 ' Uchumi wa viwanda uzingatie haki,maslahi na heshima ya wafanyakazi'
Wafanyakazi wa Acacia wakiwa wamebeba bango
Maandamano yanaendelea
Wafanyakazi wa Acacia wakiwa katika maandamano
Maandamano yanaendelea
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wafanyakazi katika viwanja vya Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro wakati wa sherehe za Mei Mosi mwaka 2017.
Baadhi ya wabunge wakiwa jukwaani
Baadhi ya wafanyakazi wa Acacia wakiwa jukwaani
Muonekano wa banda la kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia katika viwanja vya Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro
Wananchi wakiwa katika banda la Acacia kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa na wafanyakazi wa kampuni hiyo inayomiliki migodi ya Buzwagi,North Mara na Bulyanhulu
Wananchi wakiwa katika banda la Acacia
Afisa kutoka Acacia akitoa maelezo kuhusu vifaa vya uokoaji mgodini kwa wananchi waliotembelea banda la Acacia
Wanafunzi wakiwa katika banda la Acacia kujifunza masuala ya migodi
Maonesho ya Mei Mosi 2017 katika banda la Acacia yakiendelea
Aprili 30,2017-Wafanyakazi wa kampuni ya Acacia wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya Ushirika Moshi
Picha ya pamoja
Wafanyakazi wa Acacia katika picha ya pamoja
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527