Picha: RC SHINYANGA AFUNGUA KIKAO CHA WADAU WA SEKTA YA AFYA,AZUNGUMZIA UGONJWA WA EBOLA

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack amewataka wadau wa afya mkoani Shinyanga kufanya kazi kwa uwazi ili kuepuka migongano inayoweza kujitokeza wanapotekeleza majukumu yao katika jamii.


Telack ameyasema hayo leo Jumanne May 30,2017 wakati akifungua kikao cha siku mbili cha wadau wa sekta ya afya mkoa wa Shinyanga kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.



Telack alisema ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya ni vyema wadau wakatekeleza majukumu yao kwa uwazi lakini pia taasisi na mashirika mbalimbali kujitambulisha serikalini kabla ya kuanza kutekeleza majukumu yao katika jamii.

“Mkoa wa Shinyanga una wadau wengi wa afya,naomba mfanye kazi kwa uwazi na kuzingatia maadili,lakini pia ni vyema kabla hujaanza kutekeleza mradi jitambulishe kwa viongozi wa serikali”,alieleza Telack.

Katika hatua nyingine mkuu huyo wa mkoa alimtaka mganga mkuu wa wilaya ya Kahama kuchukua tahadhali kuhusu tishio la ugonjwa wa Ebola kwani wilaya hiyo ina mwingiliano wa watu wengi na wataalam wa afya wahakikishe wanatoa taarifa mara moja endapo mtu yeyote atabainika kuwa na dalili za ugonjwa huo.

“Ugonjwa huu umeripotiwa kuwepo katika nchi jirani ya Congo ,hapa kwetu bado hatujapata taarifa za kuwepo mgonjwa wa ebola,niwaombe pia wataalam wa afya maeneo yote ya mkoa wa Shinyanga kuchukua tahadhali juu ya ugonjwa huu”,aliongeza.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume aliwaondoa hofu wakazi wa mkoa wa Shinyanga kuwa ugonjwa huo haujaingia mkoani humo na kuongeza kuwa tayari wameanza kuchukua tahadhali juu ya tishio la ugonjwa huo.

Dkt. Mfaume alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau wa afya kujitokeza kusaidia katika masuala ya dharura yanapojitokeza badala ya kujikita katika sera za taasisi ama mashirika wanayofanyia kazi.

Naye Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela alisema lengo la kikao hicho cha siku mbili cha wadau wa afya mkoa wa Shinyanga ni kuwaleta pamoja wadau wanaoshughulika na masuala ya afya ili kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya afya na namna ya kuzitatua lakini pia kufahamiana.

Miongoni mwa wadau waliohudhuria kikao hicho ni pamoja na viongozi ngazi ya mkoa,halmashauri za wilaya,Shirika la Intrahealth International,CUAMM,Save the Children,JHPIEGO ,TAWLAE,Red cross,AGPAHI,World vision,ICS,PSI,AGAPE,Pathfinder International,Good Neighbors,USAID,TAMA,IMA,Amref International,HPSS na wengine wengi.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio yaliyojiri katika kikao cha wadau wa afya mkoa wa Shinyanga siku ya kwanza May 30,2017…Tazama hapa chini
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akitambulisha wadau wa afya mkoa wa Shinyanga katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akiwa na katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela
Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akimkaribisha mgeni rasmi,mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akifungua kikao cha siku mbili cha wadau wa afya mkoa wa Shinyanga
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akifungua kikao cha wadau wa afya mkoa wa Shinyanga
Wadau wa afya wakiwa ukumbini
Kushoto ni katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akiwa na Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa wa Shinyanga,Glory Mbia wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Kikao kinaendelea
Mganga Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Dkt. Rashid Mfaume akizungumza ukumbini
Wadau wa afya wakiwa ukumbini,kulia ni Mganga mkuu wa wilaya ya Shinyanga Dkt. Joseph Ngowi
Kushoto ni Mratibu wa Ubia na Sekta Binafsi mkoa wa Shinyanga Dkt. Daniel Isaac Mzee akiwa na mratibu wa huduma za maabara mkoa wa Shinyanga Muhdin Hamza 
Afisa Lishe mkoa wa Shinyanga Denis Madereke akitoa mada
Mratibu wa afya ya Mama na Mtoto mkoa wa Shinyanga Joyce Kondoro akitoa mada 
Afisa Ustawi wa Jamii  mkoa wa Shinyanga Lydia Kwerigwabe akitoa mada ukumbini
Kikao kinaendelea
Mwakilishi wa Chama cha Msalaba Mwekundu (Red Cross), Ansila Benedict akitoa mada katika kikao hicho
Mwakilishi wa shirika la CUAMM, Arianna Bortolani akielezea shughuli zinazofanywa na shirika hilo
Afisa Tiba na Matunzo kutoka shirika la AGPAHI Fidelis Temba akielezea kazi zinazofanywa na shirika hilo katika mapambano dhidi ya VVU na UKIMWI
Wadau wakifuatilia mada ukumbini

Kikao kinaendelea

Wadau wakiwa ukumbini
Kikao kinaendelea

Wadau wakiwa ukumbini

Kikao kinaendelea


Mjumbe akitoa mada kuhusu mfumo wa jazia dawa

Mwakilishi wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga akitoa mada
Mwakilishi kutoka shirika la Intrahealth International akitoa mada

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527