NAY WA MITEGO AMJIBU WAZIRI MWAKYEMBE KUHUSU KUTOIMBA SIASA

Rapa Nay wa Mitego amefunguka na kumtaka Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe kutoa ufafanuzi juu ya kauli yake aliyotoa kuwa wasanii wasijihusishe na masuala ya siasa.
Nay wa Mitego akiongea kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio, amesema kuwa yeye anaamini muziki ni siasa na siasa ni muziki hivyo ni ngumu kutofautisha vitu hivyo viwili, hivyo amemuomba Waziri mwenye dhamana kutoa ufafanuzi juu ya kauli hiyo na kudai yeye hajawahi kuimba wimbo wa siasa bali anaimba mambo yaliyopo kwenye jamii.

"Nachoamini mimi muziki ni siasa na siasa ni kama muziki, siasa ni maisha ya watu ambayo wanaishi kila siku na muziki pia ni maisha ya watu ambayo wanaishi kila siku kwa hiyo anahitaji kutoa ufafanuzi wa kutosha juu ya hili. Siasa ni maisha ya watu na muziki ni maisha ya watu, mimi binafsi naamini sijawahi kuimba wimbo wa siasa hata siku moja bali ninaimba maisha ya watu ambayo yanaendelea kila siku na ndiyo maana wengi wanathubutu kusimama upande wangu endapo linatokea tatizo lolote"alisema Nay wa Mitego.

Mbali na hilo Nay aliendelea kusisitiza kuwa kuna haja Waziri kutoa ufafanuzi wa jambo hilo

"Mh. Waziri anatakiwa kutoa ufafanuzi juu ya jambo hili ili watu wajue kipi hawatakiwi kuimba na kipi wanatakiwa kuimba sababu siasa ni maisha ya watu ya kila siku na muziki wa Hip hop ni maisha ya watu ya kila siku, kwangu mimi muziki wangu hauwezi kubadilika zaidi nitazidi kuongeza vitu ili nisiwaudhi watu na nizidi kuongeza idadi ya mashabiki"alisisitiza Nay wa Mitego


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527