MWANAFUNZI WA DARASA LA AWALI ABAKWA NA BABA YAKE MZAZI APATE UTAJIRI SHINYANGA

TANGAZA BIASHARA,HABARI,KAZI,MATUKIO YAKO KUPITIA MALUNDE 1 BLOG,TUPIGIE SIMU 0757 478 553 AU 0625 918 527


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro.
***
Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga linamshikilia mwanamme mmoja (55) jina linahifadhiwa kwa tuhuma ya kumbaka mtoto wake  mwenye umri wa miaka 09 ,mwanafunzi wa darasa la awali katika shule ya msingi Ngundangali wilayani Kishapu mkoani humo.

Akielezea kuhusu tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Muliro Jumanne Muliro alisema Mei 18,2017 saa nne asubuhi mwalimu mkuu wa shule hiyo alibaini kuhusu ukatili aliofanyiwa mwanafunzi huyo na baba yake mzazi mkazi wa kijiji cha Uchunga kata ya Uchunga wilayani humo.

“Mwalimu mkuu alibaini kuwa mtoto huyo amebakwa baada ya mwanafunzi huyo kulalamika kuwa amebakwa na baba yake mzazi”,alieleza kamanda Muliro.

Kamanda Muliro alisema chanzo cha tukio hilo ni imani za kishirikina na kwamba tayari mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi la polisi na mtoto amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kishapu na hali yake inaendelea vizuri.

Hata hivyo alisema jeshi hilo pia linamsaka mganga wa kienyeji aliyemshauri mtuhumiwa kubaka mtoto wake ili apate utajiri ili kila mmoja ashtakiwe kwa nafasi yake ya kihalifu.
Na Kadama Malunde- Malunde1 blog

Theme images by rion819. Powered by Blogger.