DIAMOND AMTAMBULISHA MSANII MWINGINE LEBO YA WASAFI...TAZAMA PICHA YAKE HAPA

Jana  tarahe 21, Diamond alitangaza kuwa atamtambulisha msanii mpya kutoko lebo ya Wasafi akifanya mahojiano kwa Clouds FM.

“Panapo majaaliwa siku ya jumatatu kesho, ntakuwepo kwenye LEO TENA ya Clouds fm na familia nzima ya @Wcb_wasafi tukimtambulisha Kijana mwenzetu Mwingine Mpya toka Mtaani, ndani ya @Wcb_Wasafi….. Sisi ni vijana ambao tumekulia kwenye umaskini na bado tupo kwenye kupambana namna ya kujikwamua kwenye umasikini… na ndiomaana tunajitahidi kadri ya uwezo wetu kila tukiona kijana yoyote mwenye nia na kipaji kumsaidia kwa kadri ya uwezo wetu, ili nae aweze kutambulisha kazi zake, na Pengine Mwenyez Mungu akimjaalia nae awe mkombozi kwenye Familia yake….Sio jambo Rahisi ni gumu, lakini kwa Sapoti yenu naamini tunaweza lifanikisha…Siku zote naomba mkumbuke WCB_Wasafi sio ya Diamond, ni ya vijana wote wapambanaji…na ndiomaana kila siku nawaomba Muendelee kuniombea na Kunisapoti, kwani Sapoti yenu ndio itayo nifanya hata kesho niweze kukuchukua wewe ama ndugu yako ili aje kukitambulisha kipaji chake na Mwenyez Mungu akijaalia kufikia Malengo…… USIKOSE kusikiliza Leo tena ya @Cloudsfmtz saa nne Asubuhi…Shukran🙏” Diamond aliandika  Instagram.

Hit maker huyo wa ‘Marry You’  leo kweli kamtambulisha msanii huyo mpya aitwaye Lava Lava ndani ya  kituo cha Cloud FM akiwa na Rayvanny.

Lava Lava tayari ameachia wimbo wake mpya ‘Tuachane’ akiwa Clouds FM leo. Wimbo wake pia unapatikana kwenye tovuti la Wasafi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527