KUTANA NA MSICHANA HUYU MWENYE TABIA ZA NYANI...ANAISHI MSITUNI KAMA MNYAMA

Polisi kaskazini mwa India wanachambua orodha walizo nazo za watoto waliopotea wakijaribu kumtambua msichana mmoja ambaye anadaiwa amekuwa akiishi na nyani.

Msichana huyo anadaiwa kuwa na tabia za wanyama hao na amekuwa akitembea kwa kutumia miguu na mikono.

Msichana huyo mwenye umri wa kati ya miaka 8 na miaka 10 alipatikana wiki chache zilizopita katika msitu eneo la Uttar Pradesh.

Madaktari wanasema msichana huyo hawezi kujieleza na anaonyesha mienendo na tabia kama za nyani.

Afisa mmoja wa polisi, wa hadhi ya juu alliambia BBC Hindi kwamba msichana huyo alikuwa anacheza na kundi la nyani huku akionyesha tabia kama zao, wakati polisi walipoenda kumuokoa.

Aligunduliwa na wanakijiji katika mbuga ya wanyama pori ilioko katika mpaka wa India na Nepal.

Afisa huyo wa polisi, Suresh Yadav alisema nyani waliwavamia yeye na wenzake walipofika kumchukua msichana huyo.

Madaktari wanasema alikuwa anaugua utapiamlo na pia kucha na nywle zake zilikuwa ndefu sana.

Alikuwa na vidonda mwilini na pia alikuwa hawezi kuwasiliana nao kwa njia yeyote ile . Alitembea kwa kutumia mikono na miguu yote .

Hali yake inaendelea kuwa bora na mwishowe atapelekwa kwenye shirika la watoto watakaosaidiana na madaktari bingwa kumfunza mienendo ya binadamu.

Afisa mkuu wa hospitali aliyolazwa , DK Singh alieleza BBC Hindi kuwa mtoto huyo atahamishwa na kupelekwa katika chuo cha matibabu cha Lucknow mara tu madaktari watakaporidhika na hali yake ya afya.

Huko atapata matibabu na usaidizi zaidi.

Hakimu wa Wilaya Ajaydeep Singh alimtembelea msichana huyo hospitalini na amempa jina la Forest Durga" linaloashiria shujaa wa Kihindi.

Wengi nchini India wanamfananisha msichana huyo na Mowgli, msichana aliyelelewa na mbwa mwitu katika kitabu cha Rudyard Kipling cha Jungle Book .

Haijiulikani amekuwa msituni kwa muda upi.

Madaktari wanasema msichana huyo hawezi kujieleza na anaonyesha mienendo na tabia kama za nyani.

Afisa mmoja wa polisi, wa hadhi ya juu aliiambia BBC Hindi kwamba msichana huyo alikuwa anacheza na kundi la nyani huku akionyesha tabia kama zao, wakati polisi walipoenda kumuokoa.

Aligunduliwa na wanakijiji katika mbuga ya wanyama pori ilioko katika mpaka wa India na Nepal.

Afisa huyo wa polisi, Suresh Yadav alisema nyani waliwavamia yeye na wenzake walipofika kumchukua msichana huyo.

Madaktari wanasema alikuwa anaugua utapiamlo na pia kucha na nywle zake zilikuwa ndefu sana.

Alikuwa na vidonda mwilini na pia alikuwa hawezi kuwasiliana nao kwa njia yeyote ile . Alitembea kwa kutumia mikono na miguu yote .

Hali yake inaendelea kuwa bora na mwishowe atapelekwa kwenye shirika la watoto watakaosaidiana na madaktari bingwa kumfunza mienendo ya binadamu.

Afisa mkuu wa hospitali aliyolazwa , DK Singh alieleza BBC Hindi kuwa mtoto huyo atahamishwa na kupelekwa katika chuo cha matibabu cha Lucknow mara tu madaktari watakaporidhika na hali yake ya afya.

Huko atapata matibabu na usaidizi zaidi.

Hakimu wa Wilaya Ajaydeep Singh alimtembelea msichana huyo hospitalini na amempa jina la Forest Durga" linaloashiria shujaa wa Kihindi.

Wengi nchini India wanamfananisha msichana huyo na Mowgli, msichana aliyelelewa na mbwa mwitu katika kitabu cha Rudyard Kipling cha Jungle Book .

Haijiulikani amekuwa msituni kwa muda upi.
Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527