KAGERA SUGAR, JKT RUVU WATOSHANA NGUVU KAITABA KWA SARE YA 0- 0

Na Faustine Ruta, Bukoba
Ligi Kuu Vodacom imeendelea tena Jumamosi na katika Uwanja wa Kaitaba tukishuhudia Timu ya Kagera Sugar ikitoka sare tasa ya 0-0 dhidi ya Timu ya JKT Ruvu inayoshikilia nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa Ligi kuu Vodacom msimu huu. 

Kikosi cha Timu ya JKT Ruvu kinachonolewa na Kocha wa zamani wa Simba, Kagera Sugar, Ashanti United na sasa JKT Ruvu King Kibadeni' kilionekana kukosa mbinu kuifunga Timu ya Kagera Sugar kipindi cha pili baada ya kuonekana kuwa na nguvu kwa kuingiza wachezaji waliokuwa na kasi kubwa. 

Kagera Sugar nao walikuwa wakifanya mashambulizi ya kila mara lakini hawakuweza kupata bao lolote kwenye jitihada zao zote hizo za kipindi cha kwanza na cha pili. Hadi kipindi cha pili kinalizika dakika 90 hakuna timu iliyoweza kumfunga mwenzake.
Kikosi cha Timu ya JKT Ruvu kilichoanza kupambana na Timu ya Kagera Sugar.
Kikosi cha Timu ya Kagera Sugar kilichoanza dhidi ya Timu ya JKT Ruvu leo kwenye Uwanja wa Kaitaba Mjini Bukoba na kutoshana nguvu kwa kutoka sare ya 0-0.
Mchezaji wa JKT Ruvu Hassan Dirunga akiwa chini ya ulinzi wa Wachezaji wa Kagera Sugar.
Hassani tena akiwapa shida wachezaji wa Kagera Sugar
Rashid Mandawa mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar akijiandaa kuingia wakati wa kipindi cha pili cha mchezo huo kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Vodacom. Picha/Habari na Faustine Ruta - Bukoba
Mchezaji chipukizi Mbaraka Yusuph (kushoto wa Kagera Sugar akiambaa na mpira huku beki wa JKT Ruvu akimkimbiza) kipindi cha pili.
Mbaraka Yusuph akilindwa na Wachezaji wa JKT Ruvu
Dakika 90 zilikamilika na Timu zote zilitoka bila kufungana, Kagera Sugar 0-0 JKT Ruvu.
Mchezaji hatari wa JKT Ruvu Hassan akiteta Jambo na Kocha Mkuu wa Kagera Sugar Mecky Mexime dakika 90 zilipokamilika.
Kocha wa zamani wa Simba, Kagera Sugar/Ashanti United/ Abdallah King Kibadeni(kushoto) akiteteta jambo na Viongozi wa Timu ya Kagera Sugar mtanange ulipomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Kagera Sugar imetoka sare ya 0-0 na Timu ya JKT Ruvu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527