AFARIKI KWA KUGONGWA KIBERENGE RELINI AKIENDA KWENYE MKESHA WA PASAKA SHINYANGA

NB- Pichani ni mfano wa kiberenge
Habari tulizozipata usiku huu wa Jumamosi Aprili 15,2017 ni kwamba mwanamke ambaye jina lake halijafahamika mara moja amefariki dunia kwa kugongwa na kiberenge katika reli eneo la Didia wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.


Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa mwanamke huyo alikuwa amepanda kwenye pikipiki akielekea kusali kwenye mkesha wa Pasaka katika kanisa katoliki Bugisi.

"Alikuwa amepakizwa kwenye bodaboda,mwendesha bodaboda alikuwa anakatisha relini bila kuchukua tahadhari ghafla wakaona kiberenge kikija,mwendesha bodaboda akaongeza mwendo na kuvuka reli...mwanamke huyo akaruka kwenye pikipiki na kuangukia relini kisha kusagwa na kiberenge hicho",wameeleza mashuhuda wa tukio hilo.

"Mwanamke huyo ambaye ni mke wa mwalimu wa shule ya msingi Mwanono alikuwa anakwenda kusali kanisa la Bugisi".

Tutawaletea habari kamili hivi punde...Endelea Kutembelea Malunde1 blog,Fahari ya Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527