ASKOFU GWAJIMA AKUNWA NA RAIS MAGUFULI..SASA KUNUNUA TRENI

Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema amedhamiria kununu treni ya umeme baada ya Rais John Magufuli kuonyesha dhamira ya kujenga reli ya kisasa(standard gauge).

Amesema kuwa treni hiyo itatumika siku za ibada kubeba waumini huku wakiimba nyimbo za kumtukuza Mungu.

 Lakini pia alisema atakuwa tayari kuruhusu itumike kubeba abiria wa kawaida.

Askofu Gwajima aliyasema hayo jana kanisani kwake, ambapo alieleza gharama za treni hiyo ni TZS bilioni 11 lakini hakusema ni lini hasa atainunua.

“Siku moja nilimchukua mwalimu Bihagaze, alikuwa mwalimu wangu wa Biblia, nikamwambia twende nikakuonyeshe mji wa mwanakondoo, nikamchukua na helkopta hadi shambani ambapo ni mji utakuwa na mahoteli, universities, kituo cha mafuta na kila kitu,”  alisema.

Alifafanua kuwa katika mji huo, kuna ramani inaonyesha kuwa reli inapita katikati. “Alipopaona akasema mbona kuna reli inapita katikati, nikamwambia nitanunua treni, akashangaa akaniuliza, treni ni shilingi ngapi? Nikamwambia dola milioni nne na mabehewa yake dola milioni tano hivi, akasema nikulipie? Nikamwambia nitanunua mwenyewe. Akapiga magoti kusujudu nikamwambia yapo mengi yanakuja,” alisema Askofu Gwajima huku waumini wake wakimshangilia kwa shangwe.

Ujenzi wa reli uliozinduliwa na Rais Dkt Magufuli Aprili 12 mwaka huu, utakamilika ndani ya miezi 30, ambapo kwa awamu ya kwanza utaanzia Dar es Salaam hadi Morogoro, treni ikiwa na uwezo wa kukimbia umbali wa 160km/hr. Treni itakuwa na jumla ya mabehewa 100.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527