MAGUFULI :MAKONDA CHAPA KAZI...HATA MIMI NAANDIKWA KWENYE MITANDAO KWA HIYO NIJIUZULU URAIS????


Rais John Pombe Magufuli amemtaka mkuu wa mkoa wa Dar es salaam kuendelea na kazi na kwamba yeye kama rais hafanyi kazi kwa kuambiwa na mtu kwamba afanye nini


Amesema watanzania wanapoteza muda mwingi kujadili mambo yasiyo ya msingi.

Siwezi nikapangiwa mtu,kwa sababu hata siku ya kwenda kuchukua fomu nilichukua mwenyewe,hakuna mtu aliyenishauri,niliamua mimi mwenyewe kwamba nafiti kuwa rais,kwa hiyo nitaamua mwenyewe nani anatakiwa awe wapi,akae wapi?...ni mimi ninayepanga....ninajua wamenielewa kwa hiyo wewe Makonda chapa kazi....nasema chapa kaziii"-Rais Magufuli.

"Suala la kuandikwa kwenye mitandao siyo tija kwangu,hata mimi ninaandikwa kwenye mitandao...kwa hiyo nijiuzulu urais??...Chapa Kazi..hapa kazi tu",-Rais Magufuli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527