WAZIRI NAPE : TUKIO LA MAKONDA KUVAMIA CLOUDS NI KUNAJISI UHURU WA HABARI

Waziri Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh Nape Nnauye amesema kuwa Tukio la Uvamizi wa Kituo cha Habari cha Clouds unaodaiwa kufanywa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Paul makonda akiwa na askari kadhaa ni tukio la kupingwa huku akidai kuwa matukio kama hayo hutokea pindi nchi inapotaka kupinduliwa lakini kama Rais yupo, nchi haijapinduliwa.

Aidha amesema kuwa Vitendo hivyo ni kunajisi uhuru wa habari na kama akishindwa kusimamia hilo na yeye hafai kuwa katika nafasi aliyopo.

Waziri Nape: Kabla ya kuchukua hatua zozote, sisi kama Serikali tunataka kusikia kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda.

Nape: Wanahabari tutulie na tusubiri kusikia kutoka pande zote mbili kabla ya kuchukua uamuzi

Nape: Natoa pole kwa Clouds Media na kwa kuwa tumejiridhisha kuwa jambo hili limetokea basi tutalishughulikia

Waziri Nape: Tumeunda timu ya watu 5 kufanya kazi katika saa 24 ili wapate maelezo ya RC Makonda na ripoti hiyo itakayoletwa na Kamati ya Uchunguzi pamoja na hatua zitakazochukuliwa vitatangazwa hadharani baada ya saa 24

Waziri Nape: Kitendo kilichofanywa na RC Makonda kinanajisi Uhuru wa Vyombo vya Habari katika Nchi Huru.Mamlaka zitajua cha kufanya

Kusaga: Kama RC Makonda ataomba radhi hatuna shida naye, ataendelea kuwa rafiki!

Reginald Mengi: Tuna Rais anayependa Vyombo vya Habari, lakini mapenzi haya ayaonyeshe kwa Vitendo!

Chanzo : Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527