MWANAMME AJIKATA UUME WAKE KWA KISU BAADA YA KUOTA ANAFANYA MAPENZI NA MAREHEMU

Mkazi wa kijiji cha Kate, wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa, amejikata uume wake kwa kisu kwa hasira baada ya kuota kuwa anafanya mapenzi na mke wake aliyefariki mwaka mmoja uliopita.


Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 58 alijikata uume wake juzi majira ya saa 4:00 asubuhi akiwa amejifungia chumbani kwake peke yake.

Mwenyekiti wa Kitongoji hicho Richard Mselema, akizungumzia tukio hilo alisema kuwa, mtu huyo alikuwa akitafuta binti wa kumuoa na kuishi nae kwa muda mrefu baada ya mke wake kufariki, lakini wanawake wamekuwa wakimkataa kwa kuwa umri wake ni mkubwa.

Baada ya kufanya tukio hilo akiwa peke yake na kupata maumivu makali, mwanaume huyo alipiga yowe na watu walipofika na kumkuta anavuja damu nyingi sehemu ya uume wake huku kisu kikiwa kimetupwa pembeni, waliamua kumbeba na kumkimbiza katika Zahanati ya Kate Mission.

Kwa mujibu wa daktari wa zamu, Paul Katindi, aliyempatia matibabu katika majeraha aliyoyapata, alisema kuwa hali yake itakuwa nzuri na anaweza kuendelea na mchakato wake wa kumtafuta mwanamke wa kuoa.

“Niliamua kujikata kutokana na kuwa na uume lakini siutumii kwa kuwa sina mke wala mpenzi. Hivyo sikuona umuhimu wala faida ya kuwa nao.” Alisema majeruhi huyo alipoizungumza na mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Nkasi, Zeno Mwanakulya, ambae pia ni jirani yake, alipokwenda kumtembelea na kumpa pole.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527