MAMIA WAJITOKEZA MKUTANO WA MBUNGE GODBLESS LEMA ARUSHA...SHUHUDIA HAPA


Mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema amefanya mkutano wake wa kwanza kwa kuzungumza na wananchi wa Arusha baada ya kutoka rumande alipokuwa ameshikiliwa kwa miezi minne.


Akizungumza katika mkutano huo Lema amesema kuwa madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema watakao kuwa waoga yupo tayari kuwakana mbele ya wananchi na kama hawawezi kuwa majasiri waachanae na chama hicho. 


Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo madiwani wote wa chama hicho katika jiji la Arusha pamoja na wabunge wa simanjiro na yule wa Monduli.


Aidha mbunge huyo amesema kuwa yupo kwenye harakati za kukamilisha kukiandika kitabu chake kitakachotoka hivi karibuni chenye historia ya maisha halisi ya wafungwa waliopo gerezani bila hatia,sambamba na wale waliobambikiziwa kesi mbalimbali.


Amewataka madiwani kuwa sambamba na yeye na kuachana na kauli wanayoisema ya kuwa wapo nyuma yake kwa kila kitu anachokifanya .
Wapili kutoka kushoto ni mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ,wa kwanza kulia ni mbunge wa Simanjiro James OLemilya akifuatiwa na aliyeko kulia kwake ni Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro,akifuatiwa na Wema Sepetu,na wa kwanza kulia ni mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha Derick Magoma
Mbunge Lema akiwa na Wema Sepetu akisalimia wananchi wa jiji la Arusha
Mamia ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo leo jijini Arusha.
Na Vero Ignatus Arusha.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527