Makubwa Haya!! JAMAA AFUNGWA JELA KWA KUMNG'ATA MBWA WA MPENZI WAKE

Chihuahua, kama huyu aliyepigwa picha Japan, ndiye aliyeshambuliwa na Arroyo

Mwanamume mmoja katika jimbo la Puerto Rico ambalo linamilikiwa na Marekani amefunga jela baada ya kupatikana na hatia ya kumng'ata mwanambwa (kilebu) wa mpenzi wake na kumkata shingo.

Luis Arroyo amefungwa jela miaka saba baada ya kukiri mashtaka ya kumdhulumu mbwa na kumnyanyasa mpenzi wake.

Mwanamume huyo wa miaka 40 alimshambulia mwanambwa huyo aina ya Chihuahua ambaye alikuwa na umri wa miezi miwili katika mji wa Lares magharibi mwa Puerto Rico.

Kadhalika, alimpiga ngumi mpenzi wake tarehe 4 Februari.

Kando na kumfunga jela, Jaji Carlos Lopez Jimenez pia alimpiga Arroyo faini ya $3,000 (£2,400).

Kwa mujibu wa gazeti la El Vocero, Arroyo, ambaye hakuwa na kazi, alikuwa ameishi na mpenzi wake wa miaka 38 nyumba moja kwa miezi sita.

Mwanambwa huyo alifariki papo hapo.

Haijabainika nini kilimfanya mwanamume huyo kumshambulia mbwa huyo.

Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527