WANAFUNZI WANNE CHUO KIKUU KIU- DAR WAKIFISHWA MAHAKAMANI KWA KUMKASHFU RAIS MAGUFULI WHATSAPP

Wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Kampala(KIU) kampasi ya Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, kujibu shitaka la kusambaza picha za kumkashifu Rais John Magufuli kupitia mtandao wa kijamii wa WhatsApp.

Washitakiwa hao ni Amenitha Kongo(19), Maria Tweve (20), Agnes Gabriel(21) na Anne Mwansasu(21), ambapo wamepandishwa mahakamani hapo leo na kusomewa shtaka linalomkabili mbele ya Hakimu Mkazi Catherine Kiyoja.

Kwa pamoja washtakiwa hao wanadaiwa kuchapisha picha ambazo zinaonyesha Rais Magufuli akiwa amevaa hijabu kama mwanamke wa Kiislamu na kuzisambaza kwenye mtandao huo wa WhatsApp, huku wakijua kufanya hivyo ni kinyume cha sheria.

Washtakiwa wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kitimiza masharti ya dhamana.

Chanzo: Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527