MSANII NAY WA MITEGO ATANGAZA KUANZISHA KANISA LAKE...HAPATAKUWA NA UTOAJI SADAKA

Nay wa Mitego anasema anafungua kanisa lake la kumuabudu Mungu. 

Amedai kuwa kanisa lake litakuwa si la biashara, bali la kumuadu mwenyezi Mungu aliye hai.

“Acha kanisa likamilike, mwenye Mungu asimamie tutajua nini kinaenda kutokea lakini sio kanisa kwa ajili ya kupiga hela,” Nay aliiambia E-News.

Nay amedai kuwa mchungaji wa kanisa lake atakuwa tofauti na hatotegemea sadaka za waumini ili kuendesha maisha yake, bali kazi yake nyingine itakayoweza kumuingizia kipato.

Rapper huyo amejinadi kuwa anatarajia kupata waumini wengi kupitia kanisa lake na kwamba litakuwa chanzo cha mafanikio katika mambo yao.

Nay amedai kuwa kanisa lake litajengwa Mbezi ya Kimara jijini Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527