MEYA WA DODOMA ALIYEWATIBUA MADIWANI DODOMA AFUNGUKA...HII HAPA KAULI YAKE

Sakata la Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Dodoma Jarary Mwanyemba kutuhumiwa kuhujumu Milioni 30 za mradi wa maji imeendelea kuchukua nafasi ambapo juzi February 21 2017 Kamati ya Madiwani iliazimia kutokuwa na imani na Meya huyo ili aondolewe madarakani.

February 22 2017 Mstahiki Meya amefanya mkutano na waandishi wa habari Dodoma na kusema kuwa hayupo tayari kuzijibu tuhuma hizo kwa sasa kwasababu mchakato wa uchunguzi bado unaendelea.

Mwanyemba amesema..>>>’Nikweli mimi natuhumiwa lakini mtu anaweza kukutuhumu katika mtazamo wake binafsi, mchakato utapofikia mwisho utaeleze hatma yake‘ –Jarary Mwanyemba

‘Mimi sina uwezo wa kusema kwa sasa, nimekuwa mtumishi wa Serikali kwa miaka mingi na ninajua kitu kinaitwa siri, nachotaka kufanya kwa sasa ni kushughulika na hili lililopo sasa hivyo nimeona nimkaimishe mtu aendeshe kikao wakati nikiendelea na hili la sasa‘ –Jarary Mwanyemba

‘Tuhuma ni jambo la kawaida lakini ninachotaka kuwahakikishia ni kwamba sijawahi kuiba na ninamshukuru Mungu sijawahi kumpiga hata mke wangu na kupelekwa kwa Balozi na sijawahi kwenda Polisi isipokuwa katika kipindi hiki ‘ –Jarary Mwanyemba

‘Halmashauri yetu ilikuwa imetulia na inaongozwa vizuri sana na hata ilifikia hakuna Diwani alikuwa akitaka kuitwa kwa chama chake, mimi nayaacha haya ili Serikali ichukue upande wake pamoja na chama pia‘ –Jarary Mwanyemba

‘Mimi naomba niandike barua ya kujibu tuhuma zangu iliyonifikia kwa siri na mimi nitaiandika na kuirudisha kwa siri hivyohivyo‘ –Jarary Mwanyemba

‘Kiukweli hii aibu iliyotokea inaniuma sana ndani ya moyo, tulikuwa na amani sana ndani ya Dodoma yetu lakini amani hiyo yote imepotea kwa sasa na siwezi kuchukia kwa lolote lile lililotokea na Mungu anaendelea kunijaalia‘ –Jarary Mwanyemba.
Via>>Millardayo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527