Taarifa Kamili!! AJALI YA MAGARI MAWILI ,PIKIPIKI YAUA WATU SABA MOSHI,YUMO MWANDISHI WA HABARI NA MWENYEKITI WA CCM


ajali ccm

WATU saba wamepoteaza maisha papo hapo katika tukio la ajali ya barabarani iliyotokea leo jioni Jumapili February 5,2017 katika eneo la Mwika mpakani mwa Wilaya ya Rombo na Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro.

Waliopoteza maisha ni pamoja na Mwandishi wa gazeti la Habarileo ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Hai, Anorld Swai.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,SACP,Wilbroad Mutafungwa alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa ajali ilitokea majira ya saa 11 jioni ikihusisha magari mawili na pikipiki maarufu kama bodaboda.

“Ajali imetokea majira ya saa 11 jioni ambapo watu saba wamepoteza maisha wanne ni kutoka katika Toyota Surf T606 AQZ, mmoja katika bodaboda MC 101 ANC huku wengine wakiwa ni kwenye Fuso T343 BNL,”alisema Kamanda Mutafungwa.

Alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Mwika katika Kijiji cha Mawanjeni katika mpaka wa Wilaya ya Rombo na Wilaya ya Moshi Vijijini na kusema kuwa chanzo cha ajali hiyo inaweza kuwa ni kuharibika kwa mfumo wa Breki wa Fuso iliyokuwa imebeba ndizi ikitokea Rombo kwenda Jijini Dar es Salaam.

Swai na wenzake walikuwa wakitokea katika sherehe ya miaka 40 ya CCM ambayo kwa mkoa wa Kilimanjaro ilifanyika pia wilayani Rombo.

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama na Mkuu wa wilaya ya Rombo, Agnes Hokororo alisema ajali hiyo ilihusisha magari mawili pamoja na pikipiki moja.

Wengine waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na Anastazia Malaysia ambaye ni Mwenyekiti wa UWT Tawi la Chuo Kikuu Cha Ushirika Moshi (Mocu) na mkazi wa Shimbi, Rombo, na Edwin Msele, katibu wa hamasa Shirikisho la vyuo vikuu Moshi mjini.

Wengine ni Ally Mbaga (Mjumbe wa NEC) wilaya ya Same na mkazi wa Mwanga, mwanamke ambaye jina halijatambulika aliyekuwa kwenye gari la Fuso, mkazi wa Himo, mwanamke aliyekuwa kwenye bodaboda ambaye fuso liligonga pikipiki hiyo na mtu mwingine mmoja ambaye hajafahamika.

Hokororo amesema majeruhi ni mwanahabari Jackson Kimambo aliyekuwa dereva wa Toyota surf hali yake inaendelea vizuri akipata matibabu hospitali ya rufaa ya KCMC.

Miili ya marehemu wote imehifadhiwa chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali hiyo.

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinaeleza chanzo cha ajali hiyo ni kuwa gari la Fuso lilifeli breki na kugonga gari hilo kwa nyuma kabla ya kuiparamia na kuigonga pikipiki na kusababisha vifo hivyo. 


Angalia picha hapa chini
Anord SwaiAnord Swai enzi za uhai wake

Ujumbe Anord Swai aliotuma kwenye group la Whatsapp kabla ya kifo chake leo alasiri saa 9.20 
Marehemu Anord Swai enzi za uhai wake

ajali moshi kilimanjaro

Ajali Kilimanjaro

Picha za ajali ya mkoani Kilimanjaro

Ajali kilimanjaro

Lori likiwa limeharibika 
 Lori
Pikipiki

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527