WHATSAPP KUWEZESHA WATUMIAJI KUFUTA UJUMBE KABLA KUMFIKIA MLENGWA


MTANDAO maarufu wa kijamii WhatsApp upo katika harakati za kuwawezesha watumiaji wake kufuta ujumbe uliotumwa kabla haujapokewa upande wa pili.

Kuna wakati unaweza kutuma ujumbe fulani kwa bahati mbaya na kugundua umefanya kosa katika WhatsApp, lakini ukashindwa kuufuta kwa sababu tayari umeshatumwa na kupokewa.

Lakini kwa sasa WhatsApp imekuja na wazo la kurekebisha tukio kama hilo kwenye simu zenye mfumo endeshi wa iOS.

Katika hilo kutakuwa na program katika eneo la ‘Settings’, ambapo utatakiwa kue-‘Edit’ kisha ‘Revoke’ mchakato utakaowezesha kufuta ujumbe huo kwa wakati mara tu unapogundua umekosea.

Hata hivyo, kikubwa ni kuwa utaweza kufanya hivyo kama tu uliomfikia bado hajausoma, ikimaanisha iwapo ameshausoma hutaweza kuufuta.

Lakini hadi sasa WhatsApp hawajatoa taarifa rasmi ya lini uwezo huo utaanza kutumika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527