Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TETEMEKO KUBWA LA ARDHI LAUA WATU ZAIDI YA 10 BUKOBA,MAJERUHI ZAIDI YA 100,HABARI KAMILI IKO HAPA


 
 Leo Septemba 10, 2016, tetemeko kubwa la ardhi lenye ukubwa wa Ritcha 5.7 limeikumbuka mikoa ya Kanda ya Ziwa hasa Kagera na Mwanza na kusababisha maafa makubwa ikiwemo nyumba za watu kubomolewa.


Maeneo yalioathirika zaidi kwa Tanzania ni, Bukoba, wilaya zote za Kagera na baadhi ya maeneo ya Mwanza. Aidha baadhi ya majeruhi ambao hawakuumia sana walitibiwa na kuuhusiwa kuondoka hospitalini hapo kurejea majumbani kwao.

Mbali na Mikoa hiyo ya Tanzania, pia tetemeko hilo limeikumba baadhi ya miji na majiji ya nchini Uganda ikiwemo KampalaMbarara iliyopo Kusini Mashariki mwa nchi hiyo.



Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mjini Bukoba, imeeleza kuwa watu 10 wamepoteza maisha kuokana na tetemeko hilo huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa vibaya na mpaka sasa wanaendelea kutibiwa hospitalini hapo.
   Kwa upande wa Mamlaka ya hali ya Hewa Tanzania (TMA) wao walitoa taaifa kupitia tovuti ya mamlaka hiyo kuwa “Leo Septemba 10,2016 hakuna tahadhari yoyote ya Hali mbaya ya hewa.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com