MSICHANA MDOGO ZAIDI DUNIANI ATANGAZWA KUWA CHIFU



Chifu wa mji wa Argungu ulioko kazkazini magharibi mwa Nigeria, Hindatu Umar aliye na umri wa miaka 25
*****
Msichana mmoja mwenye umri wa miaka 25 ametangazwa kuwa chifu wa mji Argungu wa kazkazini magharibi mwa Nigeria, ikiwa ni mara ya kwanza wanamke kushika wadhifa huo.

Hindatu Umar pia anakuwa chifu mwenye umri mdogo zaidi kuwahi kuwa chifu wa mji huo katika jimbo la Kebbi lenye wakaazi wengi waislamu.

Baadhi ya wakaazi wa eneo hilo wamelalamika wakidai hana ujuzi wa kutosha na si mkakamavu.

Lakini ukweli ni kwamba amekuwa akihudumu kama naibu wa chifu kwa muda sasa ndipo akapandishwa cheo baada ya muda wa aliyekuwa chifu kumalizika.

Mwandishi wa BBC katika eneo hilo anasema wengi wameshangazwa na hatua hiyo kwa sababu ni nadra kwa wanawake kushika nyadhfa za kiutawala na kisiasa katika maeneo yaliyo na waakaazi wengi waislamu huko kazkazini mwa Nigeria.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527