Angalia Picha: LOWASSA AWATEMBELEA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA

Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, jana amewasili Bukoba mkoani Kagera kuwatembelea na kuwajulia hali waathirika wa tetemeko la ardhi.


Tetemeko la ardhi lililotokea Bukoba mkoani Kagera Septemba 10 lilisababisha vifo vya watu 19 huku wengine zaidi ya 250 wakiachwa na maejeraha mbalimbali.


Alipofikika katika uwanja wa ndege wa Bukoba, Edward Lowassa aliyeambatana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema , Sheikh Katimba, Khamis Mgeja na Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare waliongozana hadi eneo la Hamugembe na Kashai kujionea madhara ya tetemeko la ardhi.

Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa maeneo hayo, Lowassa aliwapa pole sana kwa yote yaliowafika na kusisitiza kwamba anaamini serikali itachukua jukumu la kuwasaidia.


Aidha, amesema kuwa msaada wake yeye atampatia Mkuu wa Mkoa, Meja Jenerali Mstaafu, Salum Kijuu ili uweze kuwasaidia wananchi wa Kagera.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527