MBUNGE WA ARUSHA MJINI GOBLESS LEMA AGOMA KULA ZAIDI YA SIKU 2



Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ( Chadema) anayeshikiliwa katika mahabusu ya kituo kikuu cha Arusha Mjini amegoma kula kwa zaidi ya saa 48 sasa tangu alipokamatwa.


Lema alikamatwa juzi alfajiri akiwa nyumbani kwake Njiro Arusha kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi na kushawishi watu kwa njia ya mtandao waandamane Septemba mosi.


Jana Meya wa Arusha, Calist Bukhay alisema Lema amegoma kula akidai kuwa alifanyiwa udhalilishaji mbele ya watoto wake wakati polisi walipokuwa wakitekeleza agizo la kumkamata.


"Ni kweli amegoma kula tangu juzi alipokamatwa.Alisema askari polisi walipkwenda kumkamata walimfanyia vitendo vya udhalilishaji mbele ya watoto wake na kumnyanyasa bila kujali yeye ni kiongozi wa wananchi.

"Sasa yeye ameshikilia msimamo wake kuwa kwa kuwa polisi walikuwa wamepanga kumuua wakati wa kumkamata, basi ni bora akafa kwa njaa.


"Chakula kimekuwa kikipikwa na kupelekwa na mkewe ,lakini bado amegoma kukila.Baada ya tukio hilo, polisi walituita ili kujaribu kumshawishi ale mchana, akagoma" Alisema Meya Calist.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527