Msanii Ismail Makombe wa Vituko Show Maarufu Kundambanda Amefariki Dunia


Msanii maarufu wa Vichekesho (Komedi) kutoka kundi la Vituko Show Ndugu. Ismail Issa Makombe a.k.a KUNDAMBANDA, amefariki dunia usiku wa kuamkia leo. 
 
Huyu ni msanii wa pili kufariki dunia kutoka kundi la Vituko show baada ya Kinyambe kufariki dunia hivi karibuni.

Kundambanda alikuwa mgombea ubunge wa CUF na UKAWA kwenye jimbo la Masasi - Mtwara katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Disemba 2015 baada ya ule wa Oktoba kutofanyika kutokana na kifo cha aliyekuwa mgombea wa awali wa UKAWA, Mhe. Emmanuel Makaidi (NLD).


Katika uchaguzi huo wa Disemba 2015 Kundambanda alipata kura 14,069 dhidi ya kura 16,597 za (mshindi) Rashid Chua Chua kutoka CCM. Taratibu za mazishi zinafanyikia nyumbani kwao Masasi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527