Angalia Picha: Ajali ya Mabasi ya City Boy iliyoua Watu 29 Singida ,Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi

 
Ajali mbaya imeyohusisha mabasi mawili ya kampuni ya City Boy imetokea katika kijiji cha Maweni wilaya ya Manyoni, Singida na kusababisha watu 29 kupoteza maisha papo hapo huku chanzo cha ajali kikitajwa kuwa ni mwendo kasi na uzembe wa madereva barabarani



Mabasi hayo yenye namba za usajili T531 DCE na T247 DCD, moja lilikuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Kahama na lingine likitokea Kahama kuelekea Dar es Salaam. 



Moja ya mashuhuda wa ajali hiyo amesema kuwa madereva wa mabasi yote walikuwa katika mwendo kasi na wakati ajali inatokea walikuwa wakisalimiana kwa kunyosheana mikono kisha basi moja kupoteza mwelekeo na kuingia upande wa basi lingine na ndipo yakakutana uso kwa uso na kusababisha ajali hiyo. 



Kamanda wa Polisi Singida, Thobias Sedoyeka amethibitisha kutokea ajali hiyo na uchunguzi zaidi unaendelea kufanyika. 



Katika hatua nyingine Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi na kueleza kuwa amepokea taarifa hiyo kwa mshtuko na amesikitishwa na ajali hiyo ambayo imechukua maisha ya watanzania.
















Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527