Washiriki wa Shindano la Miss Lake zone mwaka
2014,wakiwa kwenye boti wakielekea katika hifadhi ya taifa ya kisiwa cha Saanane kilichoko mkoani Mwanza kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali-Picha na Valence Robert-Malunde1 blog
Warembo wakiwa kwenye kisiwa hicho -Picha na Valence Robert-Malunde1 blog
Warembo wakipiga picha wanyama katika kisiwa cha Saanane-Picha na Valence Robert-Malunde1 blog
Washiriki wa shindano la Miss Lake zone 2014, Jacklin Kimambo kutoka mkoa wa Kagera
akiwa na Mery Emanuel kutoka mkoa wa Shinyanga wakiwa wanatazama baadhi ya
vivutio katika kisiwa cha Saa Nane-Picha na Valence Robert-Malunde1 blog
Warembo/washiriki shindano la Miss Lake zone wakiwa katika kisiwa cha Saanane-Picha na Valence Robert-Malunde1 blog
Warembo 18 kutoka Mikoa ya kanda ya ziwa wanaoshiriki shindano la kumpata mrembo wa kanda (Miss Lake Zone mwaka 2014) wamewataka watanzania kujenga tabia ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyoko nchini na kujifunza mambo yaliyomo.
Wito huo umetolewa juzi na washiriki wa Miss Lake Zone wakati wakiwa katika kisiwa cha Saanane kilichopo katika wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza walikokwenda kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali kwenye kisiwa hicho.
Wasichana hao wameongeza kuwa watanzania wengi hawataki kutembelea mbuga za wanyama bali wamekuwa wakiwachia wageni kutoka nje ya nchi huku wakiiomba serikali kupunguza kingilio ili watanzania wengi waweze kuingia kwenye vivutio hivyo.
Wakiwa katika kisiwa hicho Mamiss hao waliweza kutembelea maeneo mbalimbali ya kisiwa hicho na kuona wanyama wanaopatikana katika kisiwa hicho ambao ni Sokwe mtu ,Tumbili, Simba mzee,Swala,pundamilia,ambao ni kivutio kikubwa katika kisiwa hicho.
Naye msemaji wa kisiwa hicho akiongea mara baada ya kuwapokea Mamiss hao Haika, Bayona ambaye ni chifu wa kisiwa hicho aliwaomba Mamiss kutangaza utalii wao wa ndani ya nchi.
Shindano la kumpata Miss Lake Zone kanda ya ziwa, litafanyika tarehe 30 mwezi huu katika viwanja vya CCM Kirumba, jijini Mwanza, ambapo mshindi wa kwanza, atajinyakulia gari la shilingi milioni 10, ambalo limetolewa na mkurugenzi wa Lenny Hotel iliyoko mkoani Geita, Leonard Bugumola.
Na Valence Robert-Malunde1 blog-Mwanza
TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA



Social Plugin