Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

STAA WA FILAMU ZA KIBONGO,PASTOR MYAMBA APATA AJALI

Taswira baada ya ajali hiyo.


STAA wa filamu za Kibongo, anayepatia zaidi kuigiza kama Mchungaji, Emmanuel Myamba ‘Pastor Myamba’ amepata ajali baada ya gari lake aina ya Toyota Creasta kugongwa na gari lingine leo mchana katikati ya Boko na Bunju jijini Dar es Salaam.




Katika ajali hiyo, hakuna mtu aliyejeruhiwa zaidi ya magari hayo mawili kuharibika.

Kwa mujibu wa Pastor Myamba, dereva aliyekuwa akiendesha gari lililogonga gari lake alitokomea na kuacha gari lake eneo la tukio baada ya kugundua kuwa ndiye aliyekuwa na makosa.
Magari yote mawili yamevutwa na 'breakdown' kisha kupelekwa kituo cha polisi Tegeta.

TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com