Happiness Kashinje enzi za uhai wake
Mazishi ya mwili wa mtoto Happiness Kashinje(9) aliyeuawa kikatili kwa kubakwa
kisha kutobolewa macho na watu wasiofahamika kisha mwili wake kutupwa kichakani
katika kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi katika manispaa ya Shinyanga
yamefanyika leo mchana katika makaburi ya familia nyumbani kwa babu yake katika kijiji cha Negezi kata ya Mwawaza
katika manispaa ya Shinyanga.
Mtoto Happinss aliyekuwa anasoma darasa la tatu katika shule ya Msingi Negezi iliyopo kata ya Mwawaza katika manispaa ya Shinyanga alikutwa ameuawa kwa kubakwa kisha kutobolewa macho juzi saa saba mchana katika kitongoji cha Kashampa kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi ndani ya manispaa ya Shinyanga
Mazishi hayo yamehudhuriwa na walimu na wanafunzi wa shule aliyokuwa anasaoma mtoto huyo,wakazi wa eneo hilo pamoja na maeneo ya jirani,wadau wa haki za watoto,waandishi wa habari,mkuu wa intelijensia mkoa wa Shinyanga,viongozi wa dini na siasa wakiongozwa na naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila.
Akizungumza wakati wa mazishi hayo yaliyohudhuriwa pia na Malunde1 blog naibu meya wa manispaa ya Shinyanga David Nkulila amelaani kitendo cha kinyama alichofanyiwa mtoto huyo huku akiitaka jamii kushirikiana na jeshi la polisi katika kuwafichua wahusika wa mauaji hayo.
Naye mkuu wa Intelijensia mkoa wa Shinyanga Bundala Maige amesema suala la ulinzi kwa watoto ni la jamii nzima na kwamba wahalifu wako ndani ya jamii hivyo kuitaka jamii kuwafichua wahalifu hao ili kukomesha vitendo vya ukatili vinavyoendelea mkoani Shinyanga.
Kwa upande wake mwinjilisti Emmanuel Donald Kaswalala aliyeendesha ibada ya mazishi alilaani vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa watotot huku akiiomba jamii kumrudia mwenyezi mungu kwa kuondokana na matendo mabaya.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
ANGALIA PICHA ZOTE ZA MAZISHI YA MTOTO HAPPINESS HAPA
TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA
TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA

Social Plugin