
Hatimaye Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA),mkoani Shinyanga kimepata viongozi wapya wa mkoa ,ikiwa imepita miaka mitatu bila ya kuwa na mwenyekiti wa mkoa wa Chama hicho.
Awali mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Shinyanga alikuwa Philip Shelembi Magadula,aliyefariki dunia mwaka 2011.
Akisimamia uchaguzi kupata viongozi wapya juzi mbunge wa jimbo la Maswa Mashariki mkoani Simiyu (CHADEMA),Sylivester Kasulumbayi(PICHANI), uliofanyika mjini Shinyanga, alisema lengo la uchaguzi ni kuendelea kuimarisha chama na kujipanga katika chaguzi za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu 2015.
Kasulumbayi aliwataja viongozi hao wapya waliochaguliwa kuwa ni Peter Frank,Mwenyekiti wa Chadema mkoa, katibu ni Zacharia Thomas, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (Bavicha), Chripin Simon, Katibu BAVICHA ni Ezekiel Joseph.
Kwa upande wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA),mwenyekiti ni Rachel Mashishanga, ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum (CHADEMA),jimbo la Shinyanga Mjini huku katibu wake akiwa ni Winfrida Daudi.
Alimtaja mwenyekiti wa Baraza la Wazee mkoa wa Shinyanga aliyechaguliwa kuwa ni Mhidini Ibrahim.
Kufuatia uchaguzi huo ambao ulifanyika kwa amani ,Kasulumbai aliwataka viongozi hao wapya (CHADEMA),mkoa kufanya kazi kwa ushirikiano bila ya kuwa na makundi ikiwemo kuzingatia sera na katiba ya Chama.
Na Marco Maduhu-Malunde1 blog -Shinyanga
TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA
TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA
Social Plugin