Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANGALIA PICHA 50 ZA TUKIO KUBWA LEO KAHAMA_MASHINDANO YA BAISKELI YALIYODHAMINIWA NA AFRICAN BARRICK YATIKISA,MAELFU YA WATU WASHUHUDIA,ZAWADI NONO KWA WASHINDI ZATOLEWA


Wakazi wa Kahama wakiwa eneo la Phantom mjini Kahama kabla   ya kuanza kwa mashindano ya mbio za baiskeli kanda ya Ziwa yaliyondaliwa na Chama cha baiskeli taifa(CHABATA) yakidhaminiwa na kampuni ya uchimbaji madini ya African Barrick.Kauli mbiu ya mashindano hayo yaliyopewa jina la "ABG CYCLE CHALLENGE" ni TUFANIKIWE PAMOJA"
-Picha na Kadama Malunde

Hapa ni katika eneo la maegesho ya malori(Phantom) mjini Kahama mkoani Shinyanga ambako mashindano ya mbio za baiskeli kanda ya ziwa yaliyondaliwa na chama cha baiskeli Tanzania(CHABATA) chini ya udhamini wa kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya African Barrick Gold(ABG) yalianzia.ABG wamedhamini mashindano hayo kusaka bingwa wa mbio za baiskeli kwa upande wa wanaume na wanawake kanda ya ziwa,ambapo takribani milioni 150 zimetolewa na kampuni hiyo kama wadau wa sekta ya michezo nchini.Pichani ni viongozi wa ABG kabla ya kuendesha baiskeli masafa mafupi kabla ya mashindano rasmi kuanza.Kauli mbiu ya mshindano hayo ni "TUFANIKIWE PAMOJA"-Picha na Kadama Malunde

Viongozi wa ABG wakijiandaa na mashindano ya mbio fupi kutoka Phantom hadi Buzwagi.Wa Kwanza kushoto ni afisa habari,michezo na utamaduni katika halmashauri ya mji Kahama bwana Kambarage Nyerere(mwenye suruali ya kijani) pia alishiriki mashindano hayo ya mbio fupi,kabla ya mashindano ya masafa marefu kwa wanawake na wanaume kutoka kanda ya ziwa inayojumuisha mikoa ya Shinyanga,Mwanza,Geita,Simiyu,Kagera,Mara na Kahama(mkoa maalum).Wanaume wameendesha baiskeli umbali wa kilomita 156.5 wakati wanawake wamekimbia umbali wa kilomita 80-Picha na Kadama Malunde

Kushoto ni Askari polisi na katibu wa CHABATA John Machemba wakipeana miongozo ya njia na usalama barabarani kwa washiriki wa mashindano ya baiskeli - Picha na Kadama Malunde

Kulia ni  katibu mkuu wa chama cha baiskeli taifa(CHABATA) bwana John Machemba akitoa maelekezo kwa washiriki wa mbio za baiskeli upande wa viongozi wa ABG,katika mashindano ya baiskeli kanda ya ziwa yaliyodhaminiwa na African Barrick-Picha na Kadama Malunde

Kulia ni mwenyekiti wa CHABATA Jax Mhagama akiendesha baiskeli katikati ni naibu waziri wa habari,vijana ,michezo na utamaduni Juma Nkamia,wa kwanza kushoto ni makamu wa rais wa African Barrick Gold Deo Mwanyika katika mashindano ya viongozi wa ABG-Picha na Kadama Malunde

Daktari wa ABG-Buzwagi  Antoinette  George akipata huduma ya kwanza baada ya kupata ajali wakati wa mbio baiskeli za viongozi wa ABG-Picha na Kadama Malunde

Viongozi wakiwa katika eneo la Phantom kabla ya mbio za baiskeli za masafa marefu kuanza.Wa kwanza kushoto ni bwana Assa Mwaipopo(General manager and Sustainability-ABG),wa pili ni makamu wa rais ABG- Deo Mwanyika,akifuatiwa na naibu waziri wa habari,vijana,michezo na utamaduni Juma Nkamia,kulia kwake ni mbunge wa Bukene Suleiman Zedi .Wa kwanza kulia ni Business Improvement Manager ABG Michelle Ash akizungumza jambo na meneja mkuu mgodi wa ABG-Buzwagi ndugu Philbert Rweyemamu-Picha na Kadama Malunde

Wakazi wa Kahama na maeneo ya jirani wakiwa eneo la Phantom kushuhudia mashindano ya mashindano ya mbio za baiskeli Kanda ya ziwa yaliyoandaliwa na CHABATA na kudhaminiwa na ABG,kampuni inayojali wananchi wanaozunguka maeneo ya migodi na sasa ukipita mjini Kahama utasikia watu wakisema"ABG ni Kahama kwanza,ABG  na Kahama,Kahama na ABG,Tufanikiwe Pamoja"
 WANAUME WA KAZI- Washiriki wa mbio za baiskeli kutoka kanda ya ziwa wakiwa tayari kuanza mbio za baiskeli leo eneo la Phantom mjini Kahama,ambapo ndipo mbio zilipoanzia kisha msafara ukaelekea eneo la Manzese kisha kwenda Tinde, na kurudi tena Kahama na kumalizia mbio hizo katika eneo la Bijampora karibu kabisa na ofisi za halmashauri ya mji Kahama.Huku wanawake wakitoka Phantom kuelekea eneo la Manzese kisha kwenda Sungamile, na kurudi tena Kahama na kumalizia mbio hizo katika eneo la Bijampora karibu kabisa na ofisi za halmashauri ya mji Kahama.-Picha na Kadama Malunde
Wakazi wa Kahama wakiwa katika eneo la Phantom kushuhudia mashindano hayo makubwa yakiwa yamedhaminiwa na ABG huku kukiwa na zawadi nono kwa washindi kuanzia wa kwanza hadi wa 30 -Picha na Kadama Malunde

Kushoto ni Katibu mkuu wa chama cha baiskeli taifa (CHABATA) bwana John Machemba akieleza historia ya mashindano ya baiskeli nchini kubwa zaidi mashindano hayo ya kanda ya ziwa ambapo mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume ameondoka na kitita cha shilingi milioni moja na laki 5 pamoja na kombe na medali huku kwa upande wa wanawake mshindi wa kwanza ameondoka na kitita cha shilingi milioni moja na laki 2 pamoja na kombe na medali.Wa pili kulia ni afisa mawasiliano mgodi wa Buzwagi bi Blandina Munghezi-Picha na Kadama Malunde

KAA SAWA_Wanaume kutoka kanda ya ziwa ambapo kila mkoa umetoa washiriki 2o,kabla kuanza mbio za masafa marefu(kilomita 156.5-Picha na Kadama Malunde

Muda mfupi kabla ya mbio za baikeli za wanaume hazijaanza-Picha na Kadama Malunde

WANAUME KAZINI_Hivi ndivyo mbio za baiskeli zilivyoanza kwa kasi ya ajabu, kila mmoja akiiwazia shilingi milioni 1 na laki 5 ya African Barrick Gold wadhamini wakubwa wa mashindano hayo yaliyoandaiwa na Chama cha baiskeli nchini Tanzania-Picha na Kadama Malunde

NI BALAA_Wanaume wakielekea Manzese kabla kuelekea Tinde -Picha na Kadama Malunde

Yaap! Mambo ya African Barrick Gold katika sekta ya michezo nchini.Pichani viongozi wa mbio hizo wakiwa sambamba kabisa na waendesha baiskeli hao leo-Picha na Kadama Malunde

SAFARI YA KUELEKEA TINDE-Nani kuibuka mshindi? -Picha na Kadama Malunde

BAHATI MBAYA_Mbio zinaendelea lakini mshiriki huyu katikati ya safari baiskeli yake inaharibika-Picha na Kadama Malunde

Wakazi wa Kahama wengi walijitokeza pembezoni mwa barabara kushuhudia mbio za baiskeli za wanaume na wanawake kutoka kanda ya ziwa-Picha na Kadama Malunde

WALIOANZA KUMALIZA NI WANAWAKE_Mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake Martha Anthony kutoka Mwanza akiingia eneo la Bijampora mjini Kahama huku akisindikizwa na kikosi maalum barabarani,huyu kaondoka na kitita cha shilingi milioni moja na laki 2,kikombe na medali-Picha na Kadama Malunde

Tunaangalia mbio za baiskeli.......-Picha na Kadama Malunde

Mshiriki upande wa wanawake akimalizia safari yake katika eneo la Bijampora-Picha na Kadama Malunde

HAWA HAWANGUI MAEMBE_Wananchi wa Nyihogo mjini Kahama wakiangalia mbio za baiskeli-Picha na Kadama Malunde

Gari likiwa limebeba baiskeli za washiriki ambao walichoshwa na safari ndefu,maana mashindano hayo siyo mchezo-Picha na Kadama Malunde

WANAWAKE WAMEMALIZA_Pichani ni askari polisi wakiandaa njia kwa ajili ya washiriki wa mbio za baiskeli upande wa wanaume ambao walikuwa wanaendesha baiskeli kwa kasi ya ajabu-Picha na Kadama Malunde

 Hakuna aliyetaka kupitwa-wananchi wakiwa juu ya mti wakiangalia mashindano ya mbio za baiskeli-Picha na Kadama Malunde
WANAUME NDIYO WANAINGIA_Mmoja wa washiriki wa mbio za wanaume za kilomita 156.5 akimaliza kwa mbwembwee-Picha na Kadama Malunde

Washiriki wakimalizia mbio hizo katika eneo la Bijampora mjini Kahama-Picha na Kadama Malunde

UWANJA WA TAIFA KAHAMA_Kulia ni bingwa wa mbio za baiskeli kanda ya ziwa bwana  Masunga Duba kutoka  Ilemela mkoani Mwanza ambaye ametumia masaa manne na dakika 13 na sekunde 58 kumaliza mbio za kilomita 156.5.-Picha na Kadama Malunde

 Mshindi wa kwanza /Bingwa wa mbio za baiskeli kanda ya ziwa bwana  Masunga Duba kutoka Ilemela mkoani Mwanza-Picha na Kadama Malunde
Mshindi wa kwanza upande wa wanawake mbio za kilomita 80,Martha Anthony kutoka Nyamagana mkoani Mwanza -Picha na Kadama Malunde

Vitendea kazi-Baiskeli zilizotumika katika mashindano zikiwa katika uwanja wa taifa mjini Kahama ambako zawadi zimetolewa-Picha na Kadama Malunde

Wakazi wa Kahama na maeneo ya jirani wakiwa uwanja wa taifa mjini Kahama wakisubiri kutangazwa kwa washindi wote-Picha na Kadama Malunde
Kulia ni afisa mahusiano mgodi wa Buzwagi bi Dorothy Bikurakule akiwa na wafanyakazi wa ABG na mwandishi wa habari katika uwanja wa taifa Kahama -Picha na Kadama Malunde

Watoa huduma ya kwanza wakitoa huduma kwa washiriki walioumia wakati wa mbio za baiskeli-Picha na Kadama Malunde

 HUDUMA YA UTOAJI DAMU KWA HIARI NAYO ILIKUWEPO UWANJANI_Kushoto ni Wakazi wa Kahama wakitoa damu,kulia ni afisa mahusiano mgodi wa Buzwagi bi Dorothy Bikurakule akipatiwa vipimo tayari kwa kutoa damu-Picha na Kadama Malunde
BURUDANI PIA ILIKUWEPO YA KUTOSHA UWANJANI_Vijana kutoka Kahama wakionesha vipaji vyao-Picha na Kadama Malunde

Mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya akimkaribisha mgeni rasmi katika uwanja wa taifa Kahama,kulia kwake ni bi Blandina Munghezi,ambaye ni afisa mawasiliano mgodi wa Buzwagi-Picha na Kadama Malunde

Mwenyekiti wa chama cha baiskeli nchini Jax Mhagama akizungumza ambapo aliipongeza African Barrick kwa kudhamini mashindano hayo hivyo kuwa wadau wakubwa katika sekta ya michezo nchini-Picha na Kadama Malunde

Makamu wa rais African Barrick bwana Deo Mwanyika akizungumza kabla ya zoezi la kutoa zawadi ambapo alisema ABG itaendelea kudhamini mashindano mbalimbali kwani inatambua umuhimu wa michezo katika jamii-Picha na Kadama Malunde

Mgeni rasmi naibu waziri wa habari,vijana ,michezo na utamaduni Juma Nkamia akizungumza na wakazi wa Kahama ambapo alisema serikali inatambua mchango wa African Barrick katika sekta mbalimbali na sasa wamegeukia michezo akasema serikali itaendelea kushirikiana kwa ukaribu zaidi na ABG katika sekta zote za maendeleo-Picha na Kadama Malunde

Mbunge wa Kahama mjini James Lembeli naye alikuwepo,yeye akaomba ABG isaidie katika kuboresha uwanja wa taifa Kahama ili uwe wa kisasa,hususani kuwekewa nyasi za bandia-Picha na Kadama Malunde

TUNASUBIRI ZAWADI ZETU_Washiriki wa mbio za baiskeli wakisubiri zawadi zao-Picha na Kadama Malunde

 Kushoto ni Business Improvement Manager ABG Michelle Ash akimkabidhi bahasha yenye fedha,mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kwa wanawake Martha Anthony kutoka Mwanza alipokea fedha kiasi cha shilingi milioni moja na laki 2,kikombe na medali,mshindi wa pili alikuwa Salome Donald kutoka Shinyanga aliyeondoka na shilingi laki 8,kikombe na medali huku mshindi wa tatu akiwa ni  Laurencia Luzuba kutoka Mwanza aliyeondoka na laki 6,medali na kikombe,mshindi wa 4 hadi 11 waliondoka na shilingi laki 2 na nusu kila mmoja na waliosalia hadi 20 wakaondoka na kifuta jasho cha shilingi laki moja na nusu kila mmoja-Picha na Kadama Malunde

Bingwa/Mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kwa akina mama Martha Anthony kutoka Nyamagana mkoani Mwanza akionesha zawadi zake-Picha na Kadama Malunde

 Mshindi wa pili upande wa wanaume bwana  Seni Konda kutoka Shinyanga akipongezwa na naibu waziri Nkamia.Konda aliondoka na kitita cha shilingi milioni moja,kikombe na medali,huku mshindi wa kwanza akiwa ni Masunga Duba kutoka kwanza aliyendoka na milioni 1 na nusu,medali na kikombe na mshindi wa tatu Simon Mbaruku kutoka Simiyu akiondoka na laki 7,kikombe na medali,wakati mshindi wa 4 hadi 10 wakiondoka na laki 5 kila mmoja,wa 11 hadi 20,wakiondoka na laki 2 na nusu na 21 hadi 30 kila mmoja aliondoka na laki moja na nusu-Picha na Kadama Malunde
 Mshindi wa kwanza ,Masunga Duba kutoka kwanza aliyeondoka na milioni 1 na nusu,medali na kikombe akishikana mkono na naibu waziri baada ya kumkabidhi zawadi-Picha na Kadama Malunde
Picha ya pamoja washindi 6,kanda ya ziwa 2014,wafanyakazi wa African Barrick na viongozi a serikali na wanasiasa akiwemo mbunge wa Kahama mjini James Lembeli-Picha na Kadama Malunde

Baada ya zawadi kutolewa burudani ikaendelea.Pichani ni msanii Dirrector Sheby akifanya yake jukwaani-Picha na Kadama Malunde

TAFADHALI BOFYA HAPA U LIKE PAGE YETU TUKUTUMIE "HABARI" MOJA KWA MOJA KILA ZINAPOTOKEA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com