
Shirika la Reli Tanzania (TRC) Kanda ya Tabora limezindua rasmi Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yaliyofanyika katika stesheni ya MGR Mkoani Tabora.
Akizungumza katika hafla hiyo Meneja wa Usafirishaji Tabora Bw. Daudi Kallogi, amesisitiza umuhimu wa kwenda hatua ya ziada katika kuwahudumia wateja na kuboresha uzoefu kwa wahudmu hasa wanapotumia huduma za reli.
Kwa upande wake muwakilishi wa Stesheni Masta kanda ya Tabora Bw. Abubakar Kitundu amesema kuwa TRC itaendelea kuweka mahitaji ya mteja katika kiini cha utoaji wa huduma.
Maadhimisho hayo yenye kaulimbiu “Going the Extra Mile” yameambatana na utoaji wa vyeti na zawadi kwa watendaji/wateja waliofanya vizuri, ukataji wa keki pamoja na burudani na picha ya pamoja.
Maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja yameambatana kaulimbiu “Going the Extra Mile” inalenga kuimarisha utamaduni wa huduma bora, kusikiliza mahitaji ya wateja na kuhakikisha TRC inaendelea kutoa huduma zinazokidhi matarajio ya watumiaji wake.











Social Plugin