Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KATAMBI, KOMBO WAKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA SHIRIKA LA IOM


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Mahmoud Thabit Kombo wamekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji(IOM),Amy Pope ambaek ameongozana Mkurugenzi wa Kikanda wa Pembe ya Afrika na Afrika Kusini,Frantz Celestin na Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji(IOM)Tawi la Tanzania,Ashraf Hassan na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Shirika la Uhamiaji(IOM),Mohammed Abunajela.

Ujumbe wa Tanzania pia umewakilishwa na Kamishna wa Uhamiaji Zanzibar,Hassan Ali Hassan,Mwakilishi wa Kamishna Jenerali wa Uhamiaji,Kamishna wa Divisheni ya Sheria,Novaita Mrosso.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji(IOM),Amy Pope yuko nchini kwa ziara ya kikazi ambapo atakutana pia na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwaajili ya kupewa Mikakati Mipango ya Nchi, Utekelezaji wa mambo mbalimbali na IOM kupokea ushari na mitazamo chanya toka kwa Mhe. Rais kuhusu maboresho na ufanisi wa kazi zao na kuimarisha ushirikiano, leo tarehe 17/8/2026,Visiwani Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) Bi. Amy E. Pope, tarehe 17 Agosti,2026 Ikulu Ndogo, Zanzibar.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com